MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

30.07.2017: MAMA AMSHUKURU MUNGU KUPATA MTOTO BAADA YA KUKAA MIKA 10 BILA MTOTO LAKINI ALIPOOOMBEWA NA BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE, YESU AKAJIBU

Baada ya kuhangaika kwa muda wa miaka 10 bila kupata mtoto, Mungu aliweza kusikia kilio chake na kumshangaza....Dada huyu aliweza kufika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na kukutana na mtumishi wa Mungu Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akiwa na kilio cha kupata mtoto, mtumishi wa Mungu alimuombea na kumtamikia maneno ya baraka. Siku ya Jumapili 30.07.2017 aliweza kushuhudia kwa furaha jinsi Mungu alivyoweza kumsaidia kupata mtoto. Alimshukuru sana Mungu, Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa maombi yake, Mch. Noah Lukumay kwa kumtia moyo na kumuombea pamoja na wachungaji wa watumishi wote wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Pengine unapitia changamoto kama za huyu dada, umehangaika sana na hujaona suluhisho la majibu yako. Nataka nikwambie kuwa yupo Mungu anayejibu, wewe endelea kumtumikia Mungu na ipo siku utaona akikuinua katika tope ulilonasa. Karibu Mlima wa Moto Mikocheni "B" na utaona Mungu akiliondoa tatizo lako moja baada ya jingine. Endelea kumtumikia Mungu, kutenda mema, kuwa mtoaji, kuwapenda watu wote, kusaidia wasiojiweza, kusoma Neno la Mungu na kulifanyia kazi, kutubu dhambi zako kila kuitwapo leo, kushiriki ibada bila kukosa, kuwatii watumishi wa Mungu, uwe mtu wa imani, usikate tamaa bali songa mbele

Nikukaribishe katika ibada ya Jumapili hii kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola.


0