RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

30.07.2017: MAMIA YA WATU WAOKOKA KATIKA IBADA YA "KUUNGANISHA NYUMBA ZETU NA MUNGU" ILIYOFANYIKA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI

Siku ya Jumapili 30.07.2017 katika ibada ya "KUUNGANISHA NYUMBA ZETU NA MADHABAHU YA MUNGU" iliyofanyika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, watu wengi sana walijitokeza madhabahuni kwaajili ya kuokoka. Wachungaji waliwaombea, wakawaongoza sala ya toba na baadae walibatizwa kwa maji mengi. Siku ya Jumatatu na Jumanne ni siku zao za kuanza masomo yao ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Wakati wanaombewa, baadhi yao mapepo yalianza kuwasumbua na kuanza kupiga kelele huku yakitaka kuondoka kutokana na moto wa Mungu ulivyokuwa ukiyaunguza. Mungu aliweza kushusha nguvu zake, na watu hawa wakakombolewa na kuwekwa huru. Hakika Mungu ni mwema sana, tunamuona akiwahudumia watu wake kupitia watumishi wake wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Yawezekana na wewe unatamani kuokoka lakini kuna sauti inasema, "USIOKOKE", nakusihi uikatae hiyo sauti kwani ni sauti ya shetani inayotaka wewe uzidi kuteseka. 

Maisha yako yamekuwa ni maisha ya kubahatisha, huna uhakika na kesho yako itakuwaje, magonjwa na mikosi imekuandama, kila ukipata pesa haitulii, kila kukicha wewe ni kilio. Pengine wewe una mali nyingi sana na ni tajiri, lakini hufurahii utajiri wako kutokana na kukosa amani katika ndoa yako, madeni yamekusonga, magonjwa yamekuandama, umetengwa na ndugu zako, hupati mume au mke wa kuishi naye, mapepo na majini yameweka makao katika nyumba yako, unaota ndoto chafu, hufurahii mali zako, hulali kitandani, ajali zinakukumba kila kuitwapo leo, roho za ukahaba zimekuandama, hutamani kusoma Neno la Mungu na mengine kama hayo. Nataka kukuambia leo, "NJOO KWA YESU, UTAFURAHIA MAISHA YAKO NA MALI ZAKO", haina maana kuona una mali nyingi lakini unaishi maisha kama ya mtu maskini, huna furaha na mali zako. Na wewe ambaye hujajaliwa kuwa na mali na hujaokoka, haina maana kuteseka duniani kwa kukosa amani kutokana na changamoto za maisha na baadae kuikosa MBINGU. Jamani njoo kwa Yesu, amueni kuokoka sasa. 

Wewe unayetamani kuokoka sasa, jitahidi Jumapili hii saa 3 asubuhi tufike katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", utakutana na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na jopo la wachungaji nao watakuongoza sala ya toba, watakuombea na utabatizwa siku hiyo hiyo.

Usafiri wa kufika kanisani ni bure kabisa kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. baada ya ibada utarudishwa kituo. Mungu akubariki sana.
Mch. Manunga


































Comments