RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BREAKING: Spika karidhia kuvuliwa Uanachama Wabunge 8 wa CUF


Siku moja baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kupokea barua kutoka kwa Mwenyekiti wa CUF Taifa anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili, Prof. Ibrahim Lipumba inayoeleza kuwafukuza uanachama Wabunge wanane wa Viti Maalum na Madiwani wawili, Bunge limeridhia.

Leo July 26, 2017 taarifa kutoka ofisi ya Bunge imeeleza kuwa Spika Job Ndugai ameridhia kufutwa uanachama kwa Wabunge hao na hivyo nafasi zao ziko wazi.

Prof. Lipumba alitangaza kuwafuta uanachama Wabunge wanane na Madiwani wawili kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya kinidhamu, kukihujumu chama, Kumkashifu na kumdhalilisha Mwenyekiti.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Spika Ndugai amejiridhisha kuwa Wabunge hao wamefutiwa uanachama kulingana na taratibu za chama hicho na hivyo hawana sifa za kuendelea na Ubunge.

Hivyo kwa mamlaka aliyonayo kwa kuzingatia kifungu cha 67(1)(b) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 kikisomwa pamoja na kifungu 37(3) cha Sheria ya Uchaguzi Sura ya 343 kama ilivyojadidiwa Mwaka 2015, Spika ametangaza nafasi hizo kuwa wazi na kumuandikia Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi aendelee na hatua zinazostahili kujaza nafasi hizo kwa mujibu wa Sheria.




Comments