MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

millardayo.com AYOTVMAGAZETIBURUDANIMICHEZOSIASAZAIDIKURASAMKITO MICHEZO PICHA: Ujerumani imetwaa Kombe la Mabara vs Chile


Wiki mbili za michuano ya Kombe la Mabara iliyokuwa inaendelea kuchezwa nchini Urusi, imemalizika leo kwa mchezo wa fainali uliyokuwa unazikutanisha timu za taifa zaUjerumani dhidi ya Chile kuchezwa katika uwanja wa Estadio Krestovski.


Timu ya taifa ya Chile ambayo iliingia hatua ya fainali kwa kuifunga Ureno imekubali kipigo cha goli 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Ujerumani iliyoingia hatua hiyo kwa kuitoaMexico, goli la pekee na ushindi la Ujerumani lilifungwa na Lars Stindl dakika ya 20 ya mchezo.


Ushindi huo sasa unaifanya timu ya taifa ya Ujerumani kuwa Mabingwa wa Kombe la Mabara wakati nafasi ya pili ikiwa ni Chile na nafasi ya tatu imewaangukia timu ya taifa ya Ureno ambayo imepata nafasi hiyo baada ya kuifunga timu ya taifa ya Mexico katika mchezo wa mapema kwa magoli 2-1.VIDEO: All Goals Taifa Stars vs Lesotho June 10 2017, Full Time 1-1
0