MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

Miss TZ Diana na Kampeni ya ‘Dondosha Wembe’ kuwanusuru Watoto wa kike
Moja ya sababu zinazotajwa kuwarudisha nyuma Wanawake ni ukeketaji ambapo kampeni na harakati mbalimbali zimekuwa zikifanywa kuhakikisha Mwanamke anathaminiwa na kupewa heshima yake.

Miongoni mwa watu waliokuwa na shauku kuhakikisha Mwanamke anakuwa na hadhi ni pamoja na Miss Tanzania 2016 Diana Edward ambaye ana Kampeni yake inayoitwa “Dondosha Wembe” ikiwa na lengo la kupinga vitendo viovu kwa wasichana hasa wa shule ikiwemo ukeketaji, ubakaji na unyanyasaji kijinsia.

Leo July 28, 2017 Kampeni hiyo imewafikia Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwandeti iliyopo Ngaramtoni, Arusha ambayo inaelezwa zaidi ya 75% ya Wanafunzi wa kike wamefanyiwa vitendo vya ukatili ikiwemo kukeketwa.

0