MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

Mwili wa mtoto wa miaka 3 umekutwa na sindano 7 zilizoingizwa kishirikinaWanasema tembea uone au subiria usimuliwe…yapo mambo ambayo hutokea katika maeneo mengi ya dunia hii – mambo ambayo mara nyingi hayaaminiki ila kwa baadhi ya watu.

Mtandao maarufu wa Daily Mail leo July 28, 2017 umeripoti kuwa mtoto wa kike aliyekuwa na umri wa miaka mitatu amefariki baada ya kutumiwa kichawi na boss wa mama yake ikiwemo kunyanyaswa kijinsia.

Mtoto huyo aliwahishwa Hospitalini katika mji wa Kolkata, Magharibi ya Bengal akiwa katika hali mbaya ambako baada ya kufanyiwa uchunguzi aligunduliwa kuwa na sindano saba katika mwili wake zilizoingizwa kishirikina.

Taarifa ya Polisi inasema kwamba mtu anayeitwa Sanatan Thakur, ambaye hujihusisha na masuala ya nguvu za giza alimuajiri mama wa mtoto huyo kumfanyia kazi za ndani na kumtumia mtoto huyo katika mambo ya kishirikina.

Ingawa Madaktari walifanikiwa kuziondoa sindano zote saba, mtoto huyo alifariki.

0