RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

Tamko la Serikali kuhusu homa ya Ini, yasema “Wananchi wapo hatarini”



Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameeleza mipango ya Serikali katika kukabiliana na homa ya Ini akisema chanjo ya homa hiyo itapatikana kwa wananchi wote waliokuwa kwenye hatari ya kupata ugonjwa huo au walioupata ugonjwa huo bila kujali kigezo cha umri wala uwezo wa kifedha hadi kufikia 2020 kutoka mwaka wa fedha 2018/2019.

Aidha, Waziri Ummy amesema kwa sasa hakuna mlipuko wa ugonjwa huo lakini ametoa angalizo kuwa Wananchi wa Tanzania na Afrika Mashariki wapo katika hatari ya maambukizi ya ugonjwa huo.

Comments