RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

20.08.2017: FURAHA ISAYA AKONGA MIOYO YA WATU KATIKA IBADA YA KUFUNGUA MILANGO MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Siku ya Jumapili 20.08.2017 tumebarikiwa sana na huduma ya Furaha Isaya kwa wimbo wake wa "AMENIHURUMIA" alioimba katika ibada ya KUFUNGUA MILANGO ILIYOFUNGWA NA MAADUI ZETU ILI TUSIFANIKIWE, ibada hii iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. 

Kupitia wimbo wake tuliona uwepo wa Mungu katika ibada hii ya kihistoria. Hakika Mungu ameweka kitu ndani yake, tumeona Mungu akishughulika na mioyo ya watu kwa ujumbe mzito aliouweka ndani ya Furaha Isaya. 

Watu wengi walijitokeza madhabahuni kumtunza na kumtia moyo mwimbaji huyu kutokana na  jinsi walivyokuwa wakiguswa na ujumbe wake mzito ambao Mungu aliweka ndani yake. Mungu azidi kumtumia Furaha Isaya ili watu waokoke na wamtumikie huyu Yesu Kristo. Yawezekana ungetamani mwimbaji huyu aje akuhudumie katika huduma yako, unaweza kuwasiliana naye katika facebook akaunti yake ya Furaha Isaya​ naya atakupa ratiba nzima ya huduma yake.

Furaha Isaya ni muumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na ni mwimbaji katika Praise & Worship Team ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" tangia akiwa  mtoto mpaka sasa. Kwahiyo muombee ili asonge mbele kwa kazi ya BWANA, iombee familia yake, huduma yake na karama yake, kazi zake n.k 

Tunakukaribisha katika ibada ya Jumatano saa 9 alasiri, Ijumaa saa 9 alasiri na Jumapili saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Siku ya Jumapili usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, na baada ya ibada utarudishwa kituoni. Njoo na rafiki yako.

Furaha Isaya












Comments