RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

20.08.2017: WAUMINI WALIVYOMTUKUZA MUNGU KWA NYIMBO NA KUCHEZA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI

Leo natamani nikupe faida chache za KUMSIFU MUNGU kama watumishi wa Mungu wa Mlima wa Moto Mikocheni "B" wakishirikiana na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare walipoamua kumsifu Mungu kwa njia ya nyimbo katika ibada ya KUFUNGUA MILANGO ILIYOFUNGWA NA MAADUI ZETU ILI TUSIFANIKWE iliyofanyika siku ya Jumapili 20.08.2017.

Sifa au kusifu Mungu maana yake nini?

a)Kumsifu Mungu ni kuongea, kukiri, au kushuhudia na kuimba kuhusu Uweza wa Mungu, nguvu za Mungu, Mamlaka ,matendo makuu aliyotenda Bwana (kazi zake), miujiza, mambo ya ajabu, uumbaji na nafasi ya Mungu katika maisha yetu na uhusiano wa Mungu na wanadamu. Kwa mfano: (Mungu ni Mfalme: Wewe ni Mfalme, Baba yetu, U Bwana , Ni muumbaji wetu, ni Mchungaji, mponyaji, ni wa kwanza na wa mwisho ( Alfa na Omega) na mtoa mahitaji yetu kama majina yake yanavyomtambulisha .Una nguvu, umeumba mbingu nchi na vilivyomo, mtenda mijuza, unaweza yote, umetuponya, umetulinda, Mungu katupigania [zaburi 150:1-6]. mistari hii inaeleza tumsifu Mungu wapi, kwa nini na namna gani au kwa kutumia nini.

b)Pia sifa ni namna mojawapo ya kujitoa sisi wenyewe kwa Mungu kama sadaka (dhabihu za sifa), ni kumuenzi na kumkubali, Mungu ni nani na aliyoyatenda kwa mioyo yetu, nafsi , akili, nguvu na miili yetu yote inatakiwa ihusike. [Waebrania 13:15] “Basi kwa njia yake yeye na tumpe Mungu dhabihu za sifa daima yaani tunda la midomo liungamalo jina lake .
[Warumi 12:1-2] “Basi ndugu zangu nawasihi kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu yenye kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana”.

Imefika kipindi cha sasa tunatakiwa tuache kuahidi kumsifu Mungu kama Daudi aliposema “nitakutukuza, nitamwimbia Bwana, kwani alikuwa katika vita na kutangatanga porini akimkimbia Sauli hivyo alikuwa akiahidi kumsifu Mungu atakapookoka . Sifa zenye mguso kwa Mungu ni zenye maneno ya kumwambia Mungu moja kwa moja kama vile unamuona au unaamini yupo hapo unapoimba au kutamka sifa zake...”Ninakuimbia Bwana, ninakusifu mfalme..

Ni maombi yangu kwamba kitabu hiki kitakutoa katika, desturi za ibada, mapokeo ya kipentecost au liturgia na udini uliowafunga wakristo wengi, kitabu hiki kikusaidaie kupata uamusho wa kiroho na kuifanya huduma ya kusifu na kuabudu kuwa sehemu au mtindo wa maishayako ya kila siku. Kwani kusifu na kuabudu ni mahali popote, wakati wowote na hata ukiwa peke yako. “ Mfalme Daudi alisema [ zaburi 146:1-2] Nitamsifu Mungu ningali hai, muda ninaoishi.” Aliamua kumsifu Mungu asubuhi, mchana na usiku mara saba kwa siku. Akapewa jina la “mtu autafutaye moyo wa Mungu”..
Kumbuka huduma zote zitakoma hapa duniani isipokuwa kusifu na kuabudu kutaendelea mbinguni milele na milele lazima uipende na kuanza kuifanyia mazoezi huduma ya sifa na kuabudu kwa kuienzi na kutoa muda zaidi. Kwani ibilisi anaipiga vita huduma ya sifa na kuabudu anajua ni kiboko kwake ndio maana amewafunga waumini wengi wasiienzi .

Leo ngoja tuishie hapo, lakini pengine ungetamani kushiriki ibada ya Jumapili hii itakayoanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana na hujui utafikaje. Kanisa letu lipo Mikocheni "B" na limeandaa usafiri wa bure wa kufika kanisani kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa, ukifika hapo utaona magari yetu. Baada ya ibada kuisha utarudishwa kituoni bure kabisa.

Usisahau kuja na rafiki yako au ndugu yako














Comments