RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

27.08.2017: MCH. NOAH LUKUMAY AGUSA MAISHA YA WATU KATIKA IBADA YA TAMASHA LA MAOMBI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI

Mungu ni mwema na mwenye huruma kwa kila amtafutaye kwa bidii. Siku ya Jumapili 27.08.2017 tumeona wema wake kupitia mtumishi wake Mch. Noah Lukumay wakati akihubiri Habari Njema katika ibada ya Tamasha la Maombezi iiliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" linaloongozwa na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.

Ujumbe wa Mungu kupitia kinywa cha mtumishi wake Mch. Noah Lukumay ulipenya katika nafsi za watu. Tunamshukuru sana Mungu kwani kwa kupitia mahubiri hayo watu wengi sana waliweza kufunguliwa katika mitego ya shetani na majaribu waliyokuwa wakipitia. Tuna kila sababu ya kujivunia wokovu tulionao kwasababu tuaona jinsi Mungu anavyofanya mambo makubwa kupitia huduma yake ya Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Mch. Noah Lukumay baada ya kumaliza kuhuhibiri Habari Njema aliweza kufanya maombi kwa watu wenye shida mbalimbali kama vile wenye uhitaji wa watoto, uponyaji, kupata kazi, kupandishwa vyeo, kuinuliwa katika huduma zao, kufaulu masomo, kuondolewa nguvu za giza, kuondolewa mapepo na majini, kuondolewa roho chafu, kuondolewa ndoto mbaya, na mengine kama hayo. Wakati wakiombewa watu wengi walifunguliwa na tuliona ukuu wa Mungu.

Mungu amekuwa mwaminifu sana katika huduma hii ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwani tunaona watu wengi wakishuhudia jinsi Mungu alivyowatendea miujiza baada ya kuombewa na mtumishi wake Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Mch. Noah Lukumay na wachungaji mbalimbali wa kanisa hili. Mungu amekuwa akiwatimizia yale wanayoyaomba kwa wakati aujuao Yeye.

Yawezekana una hitaji lako na unatamani Mungu akusaidie kwa njia moja au nyingine ili uwekwe huru na ufuarahie ukuu wa Mungu kwani kwa kipindi kirefu umekuwa ukiteseka na kuonewa. Jitahidi kufika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ukiwa na imani ya kupokea majibu yako kutoka kwa Mungu wetu wa mbinguni, kupokea baraka tele. Unachotakiwa kukifanya ni wewe, kujitakasa uingiapo kanisani, kuungama dhambi zako na kutozitenda tena, kuwa msikivu kanisani na kuyafanya yale unayofundishwa na watumishi wa Mungu, kusoma Neno la Mungu na kuyaishi yale unayoyasoma katika itabu vitakatifu vya Mungu, kuwa na imani kwa kila jambo unalofanya na unaloambiwa na watumishi wa Mungu au kwa kusoma Neno la Mungu, ku jituma katika kusapoti huduma kulingana na kile unachobarikiwa, kuwa na upendo kwa kila mtu, kusaidia wenye uhitaji, kutenda yaliyo mema; ukifanya hivyo utaona mkono wa Mungu katika maisha yako...

Pia tunapenda kuwajulisha kuwa tupo katika maadalizi ya somo la Mch. Noah Lukumay kwahiyo endelea kufuatilia post zetu.
Ibada zetu za Jumapili zinaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa, utaona magari yetu. Baada ya ibada 
utarudishwa kituoni.

Mch. Noah Lukumay



Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare




Mch. Stanley Nnko





Mch. Elizabeth Lucas















































































Comments