RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

27.08.2017: UJUMBE WA BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE KUHUSU SIKU ZA MWISHO

Siku ya Jumapili 27.08.2017 Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kuhubiri mambo mbalimbali kwenye tamasha la Maombezi lililofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B”. Vitu alivyohubiri ni kama vifuatavyo:-

SIKU ZA MWISHO NI SIKU ZA HATARi
2Timotheo 1-5: Siku za mwisho ni siku za hatari, na dalili mojawapo ya za siku za mwisho ni watu kuzipenda fedha kuliko kumpenda Mungu, hawana suluhu, watapenda mambo ya anasa, hawasamehe. Katika siku hizi za hatari sisi kama Wakristo tunatakiwa kujitakasa, tukumbushane kwa yale ambayo hayastahili mbele za BWANA nay ale yanayostahili mbele za BWANA ili watu waweze kuingia mbinguni.


KUOKOKA KWAKO KUSIISHIE KANISANI BALI UFIKE MBUNGUNI.
Ni furaha yangu nikukute mbinguni, nikushike mkono wako tukiwa wote mbinguni tukifurahi, tukishangilia kwa pamoja. Nakuomba ukae katika kivuli cha kanisa hili la Mlima wa Moto mpaka tutakapoingia mbinguni. Usiache kufika kanisani. Nitasikitika sana kukuona unaachwa kwenda mbinguni na unaelekea jehanamu ile siku ya hukumu, wakati tukiwa duniani tulihangaika wote, tulikesha wote kanisani, tulicheza wote madhabahuni, tuliimba wote, tulitiana moyo, tulielimisha Neno la Mungu wote.

DALILI ZA SIKU ZA MWISHO
Siku hizi za mwisho, tunaisha katika maisha ya hatari yenye vita ni vingi, maneno mengi, masengenyo, usingiziaji, umalaya, uongo, uchawi, ulawiti, kiburi, kutompenda Mungu, kuuzoea wokovu, kudharauliana, kulogana, watu wanajipenda wenye mpaka wanamsahau Mungu na mengine kama hayo. Lakini ili uepukane na hayo yote unatakiwa kusimama na BWANA kwasababu kipindi hiki tulichonacho tumekalia kuti bovu. Unatakiwa kujua kuwa saa yoyote Yesu atarudi, na atakaporudi akukute uko tayari na ukiwa na imani na upendo.

SAPOTI KAZI YA MUNGU, ISONGE MBELE
Watu wengi siku hizi makanisani wamekuwa wagumu sana kusapoti kazi ya BWANA ili isonge mbele. Hawajui wanapokuja kanisani kuna vitu wanatumia ambavyo vinahitaji pesa, kwa mfano umeme, uchakavu wa vifaa vya muziki, kuwalipa wafanyakazi wa kanisa, kulipia vipindi katika televisheni mbalimbali, kulipia matangazo, kulipia maji, viti wanavyokalia n.k. Cha kustajabisha watu hawa wamekuwa wepesi sana kuchangia vitu vya mwilini na kuacha mambo ya rohoni, wamekuwa wepesi kuchangia harusi na sendoff bila ya kulazimishwa. Wamemtupa Mungu wao, wanamuabisha Mungu wao wanapowatesa watumishi wao kwa kuwaza jinsi gani wataipeleka injili bila hofu.

TUNAKEMEA ROHO YA KUPENDA YA MWILINI KULIKO YA MOYONI
“Leo ninavua ile roho chafu iliyokuvaa ya kupenda mambo ya mwili na kuacha mambo ya rohoni katika jina la Yesu Kristo. Ninakuvua udunia katika jina la Yesu na ninakuvaa mambo ya rohoni, ninakemea roho ya kukata tamaa, kutopenda kusoma Neno la Mungu, kutopenda kushabikia mambo ya Mungu, naondoa roho ya majivuno, roho ya kuzoea wokovu, roho ya kumzoea Mungu wako na kumfanya kama babu yako, nakemea roho ya kuridhika na tabia mbaya ya kutompenda Mungu kutoka moyoni mwako, nakemea roho ya kutotii watumishi wa Mungu, kwa jina la Yesu Kristo…Amen”

TAMANI VITU VYWA MBINGUNI UKIWA BADO UPO DUNIANI
Tamani vitu vya mbinguni ili siku ya mwisho ya kuishi ukakutane na Mungu mbinguni. Kizazi cha sasa kimetekwa na mambo ya dunia, watu wamemsahau Mungu. Siku za mwisho ni siku za hatari na hasara kwa yule asiye na Mungu ndani yake. Ni lazima ukae imara Kiroho kama wewe ni mtu anayempenda Mungu ili ukabiliane na changamoto na majaribu ya shetani. Watu wengi hawana utii kwa wazazi wao, viongozi wao au watumishi wa Mungu. Nakumbuka zamani ukiitwa na mchungaji unatetemeka lakini siku hizi unamchukulia kirahisi sana mchungaji wako. Mchungaji akiitisha kikao watu hawaendi lakini kwenye sherehe utaona watu wako mstari wa mbele. Mimi ninataka mioyo yenu ibadilike ifanyike kuwa mipya na yenye hofu ya Mungu

RUDISHA KIU YA KUPENDA KUKAA KANISANI
Ile kiu ya mwanzo ya kupenda kukaa nyumbani mwa BWANA yaani kanisani natamani irudi sasa kama kipindi cha nyuma. Wakristo wa sasa ni Wakristo wenye kifafa cha kiroho, ile kiu ya kwenda kanisani imepengua, ile hofu ya Mungu imepoa sana. Watu wanaringa sana kumtumikia Mungu. Hata ukiringa katika kazi ya Mungu, yupo atakayekushughurikia kipindi umebanwa ambaye ni Mungu aliyekuumba. Unataka kuondoa udunia katika moyo wako na kuhangaikia ya mbinguni. Watu mko “busy” kutafuta vitu vya kuvaa wapendeze, chakula washibe matumbo yao, hawaridhiki na wanachopata, kila kukicha wako “busy.” Kuridhika na kile unachopata ni faida kubwa sana kuliko kuwa na tamaa ambayo itakufikisha katika mateso. Anza sasa kuwa busy na mambo ya Mungu.

NIKUPE SIRI YA MAFANIKIO YANGU-Bishop Dr. Gertrude Rwakatare
Mimi ninampenda sana Yesu Kristo kwasababu nilivyoamua kuokoka nimeona mabadiliko makubwa katika maisha yangu yamekuwa bora. Watu wengine wanasema, “Mama Rwakatare aliolewa na Mmarekani na ndio maana alimuachia mali na sasa ni tajiri.” Watu bado hawajajua mafanikio yangu yanatokana na nini. Mafanikio yangu yanatokana na Yesu Kristo, nimekuwa mwaminifu kwake na ndio maana amenibariki na kufanya kazi kwa bidii. Mungu amenivusha kwani nilianza nikiwa chini na leo Mungu ameniinua. Mtegemeeni Mungu katika maisha yenu na kufanya yale anayowaagiza ndipo mtafanikiwa.


Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare










































Comments