RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

“Serikali iwalinde wanaojitolea kupigania rasilimali za nchi” – Wanaharakati



August 17, 2017 zilisambaa taarifa juu ya kifo cha aliyekuwa Mpelelezi kinara aliyefanikisha kukamatwa kwa Yang Feng Glan maarufu kama ‘Malkia wa Meno ya Tembo’ Wayne Lotter ambaye alipigwa risasi na watu wasiojulikana DSM.

Kutokana na kifo hicho watu mbalimbali hasa wadau wa kupinga ujangili wameitaka Serikali kuhakikisha wanafanya uchungiz wa kina kuwabaini waliohusika na tukio hilo na kuwafikisha mbele ya sheria na haki inatendeka.

Mkurugenzi Msaidizi wa Kuzuia Ujangili katika Idara ya Wanyamapori Robert Clemence amesema Serikali imejipanga kuhakikisha inawakamata wahusika wa tukio hilo lililotokea wiki iliyopita.

>>>”Kama marafiki tumejifunza kuwa ukifanya kazi lazima uwe tayari kwa lolote litakalotokea. Hii itatupa hamasa ya kuendelea kupambana zaidi na tutahakikisha uhalifu dhidi ya uuaji wa tembo tunaukomesha kabisa nchini.” – Robert Clemence.

Comments