RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

17.09.2017: WANANDOA WAMSHUKURU MUNGU KWA KUFANIKISHA HARUSI YAO

MITHALI 15:13-14- "Moyo wa furaha huchangamsha uso; Bali kwa huzuni ya moyo roho hupondeka. Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa; bali kinywa cha wapumbavu hula upumbavu"

Wanandoa hawa kabla hawajachumbiana wala kuoana mioyo yao ilikuwa na huzuni na nyuso zao zilikuwa hazijachangamka. Ila walipozidi kumuomba Mungu na kulia mbele zake, Naye aliweza kufuta machozi yao na kuyajibu maombi yao. Hivi sasa mioyo yao ina furaha na nyuso zao zimechangamka, wanamtukuza Mungu..

Mungu aliwapa ufahamu na maarifa ya kutambuana na kusomana tabia na ndio maana leo wameungana na kuwa mwili mmoja.

Pengine na wewe moyo wako una huzuni na uso wako haujachangamka kutokana na maisha ya upweke unayoishi. Kwa muda mrefu umekuwa ukitamani kuishi maisha ya ndoa lakini imeshindikana. Rafiki na ndugu zako uliosoma nao wameoana lakini wewe bado. Umebaki kuwa na huzuni. Nakutia moyo muombe Mungu akupe ufahamu ambao utakusaidia kupata maarifa ya kumpata yule umpendae. Mungu atakupa maarifa ambayo yatakusaidia kumpata mume/mke ambaye ulikuwa unamsubiri kwa muda mrefu.

Unatakiwa kutambua kuwa mume/mke wako yupo ila kwa akili ya kibinadamu humuoni ila kwa ulimwengu wa kiroho yupo. Naye anaomba siku moja akutane na wewe, kwahiyo jaribu kuwa karibu sana na Mungu naye atakupa ufahamu utakaokusaidia kupata maarifa ya kumapata mume wako/mke wako.

Katika ibada ya MAOMBI YA KUFUFUA VITU VYETU VILIVYOKUFA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto MIkocheni "B" siku ya Jumapili 17.09.2017 wanandoa hawa walimshukuru Mungu kwa kufanikisha malengo yao ya kufunga ndoa. Walimshukuru Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa malezi ya kiroho, Mch. Noah Lukumay kwa mafundisho ya ndoa na kuwafungisha ndoa, wana Mlima wa Moto wote kwa kusapoti harusi yao.

Tunakukaribisha Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho hadi Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. Baada ya ibada utarudishwa kituo walikokukuta. karibuni wote













Comments