Tunawapongeza wanafunzi wa darasa la saba kwa kufanya maafali katika shule bora Tanzania ya Morogoro Kihonda St Mary's kwa mwaka 2017. Pia tunampongeza Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare Rwakatare na MD. Rose Rwakatare kwa jitihada zao za kuhakikisha shule inapata walimu bora, masomo bora, vyakula vya kutosha, vitabu vya kutosha, wafanyakazi wenye kujituma., maktaba nzuri, viwanja vya michezo, maabala nzuri. Shule imekuwa ni moja ya shule bora Tanzania kwa kufaulisha na maadili mema kuanzia walimu, wafanyakazi na wanafunzi. Mazingira yanaruhusu mwananfunzi kujisomea na kufanya michezo mbalimbali inayopatikana katika shule hiyo.
Watu wengi wanajiunga na shule hii kutokana na historia nzuri ya kitaaluma na kimaadili. Wanafunzi mara nyingi wanapata muda mwingi wa kujisomea na kukaa na walimu wao baada ya masomo ili kuweza kuwaauliza pale ambapo hawakuelewa vyema. Shule hii imebahatika kuwa na maktaba nzuri yenye vifaa vyote vya wanafunzi kujifunzia na pia maktaba yenye vitabu vyakutosha vya kujisomea.
Comments