MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

15.10.2017: MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ATOBOA SIRI ZA WACHAWI NA WAGANGA


Siku ya Jumapili 15.10.2017 katika ibada ya KUVUNJA YA NGUVU ZA UGANGA NA UCHAWI iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikcheni “B” alikuwa na haya ya kusema, “Bwana apewe sifa. Unajua mateso ya wenye haki ni mengi lakini Mungu huwaponya nayo yote.
Zaburi 34:19. Sisi tuliyeokoka tunatembea juu ya matatizo ya ulimwengu. Hata kama unapitia katika shida na taabu lakini kumbuka unaye Mungu wa mbinguni atakayekuongoza katika njia sahihi kufikia mafanikio yako. Watu wengine hawana matumaini kila akiangalia mbele, nyuma, kulia na kushoto anaona hana msaada, lakini wewe kama mtu wa Mungu ukiona imeshindikana kulia au kusho, mbele au nyuma, basi wewe angalia juu mbinguni kwani msaada wako unapatikana kwa BWANA aliyeziumba mbingu na nchi.

Tumekuwa tukiomba na kufunga kwaajili ya magonjwa yaliyomwaga ulimwenguni yenye majina na yasiyo na majina, lakini Mungu ni mwamainifu amekuwa akisikia maombi yetu na kutujibu, kwani aliyachukua magonjwa yote msalabani ni BWANA wetu Yesu Kristo alipigwa mijeredi na sisi leo ni wazima. 

Kumekuwa na mateso mengi hapa duniani kama vile ya umaskini, uhitaji, ukata lakini bado tunayo matumaini mbele za Mungu kwani fedha na dhahabu ni mali yake.

Tumekuwa tukiombea matatizo ya watu mbalimbali kama vile matatizo ya ndoa, watoto na Mungu amekuwa akifanya mpenyo na watu wanafunguliwa. Tunawaombea watu waliofungwa kuolewa na kutupiwa majini mahaba, kwa maana jini mahaba ni shetani lenye wivu ambalo halitaki kuona wewe msichana unaolewa, unashangaa kila ukichumbiwa baada ya muda unaachwa, na pengine unabahatika kuolewa lakini linafunga uzazi usizae, na likiona mimba imeingia basi linaporomosha mimba yako.

Kuna baadhi ya watu wametupiwa nguvu za kichawi kazini kwao, mtaani kwao, nyumbani kwao, pengine ulienda kijijini wakakutupia na kila ukijaribu kufanya jambo Fulani hufanikiwi, kuna watu wengine wanaona wivu ndoa za watu wanachokifanya ni kufunga uzazi ili ukawie kuzaa. Wachawi ni agent wa shetani wanaofanya kazi ya kuvuruga amani na furaha ya watoto wa Mungu. Na ndio maana unaoa kila jambo ulilopanga litokee leo, linatokea baada ya miaka 10.

Unajua kuwa mbuzi aliyefungwa hawezi kwenda zaidi ya kamba yake. Utakuta mtu ni msomi kabisa na alitakiwa kwenda mataifa mbalimbali, lakini mchawi anafunga miguu yake na hapati safafri za Ulaya, anabaki kutumwa na bosi wake mikoani tu.

Katika uchawi, kuna wachawi waafunzi, washilikina yaani wachawi mafunzoni. Tunaona watu wengi siku za Jumamosi wanaenda kwa mafundi (waganga) kwaajili ya kuwaloga wenzao, hao tunasema ni washilikina, waharibifu. Na katika kanisa wapo watu wanaoharibu wenzao, wapo wachawi wanaoleta magonjwa kwa wenzao, waliofunga uchumi wako na kusababisha kukaa mahali pamoja, wapo waliozuia hatua zako zisiendelee mbele kwenye mafanikio yako.

Matendo ya Mitume 8:9-13 na 18. Sisi ni watoto wa Mungu kwahiyo wachawi wanapotutupia uchawi wao ukawarudie wao kwa jina la Yesu Kristo. Utakuta watu wengine wanakunyatia nyuma wakifuata unyayo wa miguuu yako ili aibe nyota yako, kibali chako ili akatembelee katika kazi zake. Watu wengi sana wameibiwa vibali vyao, nyota zao, wengine zamani walikuwa wanang’ara lakini sasa hivi wamefifia na hawasikiki kabisa, wengine walipanda kibiashara lakini hivi sasa hawawezi kushika hata Tshs, 100. Kuwa makini sana na watu wanaokuomba pesa, kwani ukiwapa tu wanakwenda kukumaliza nayo kwa wachawi.
Katika maisha yetu haya hakuna mtu asiye kuwa na adui. Unaweza kumuona mtu anakupenda kumbe anakuchukia, kwahiyo njia ya kujikwamua ni kumlilia Mungu kwani sisi hatuna waganga bali uponyaji wetu upo madhabahuni. Mungu awabariki sana.
Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

0