RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NEEMA MUDOSA ATOA YA MOYONI KUHUSU WATU WANAO "COMMENT" MAMBO YA AJABU AJABU KATIKA FACEBOOK AKAUNTI YAKE

Ninapo andika ao ku post chochote ukisoma unasikia halikuhusu pita Kimya mara moja tena utulie kama moja.en Silence kabisa kama wengine.
Maana unafikiri kua mkisto ni kua bubu ao kufanya mambo bila kufikiria.
Najua ninacho kifanya,kama kwako unafikiri napoteza mda acha nikwambie kwamba kuna maelfu ya watu wametiwa moyo na mpaka sasa wanasimama na Mungu kwa sababu tuu ya kupokea ujumbe ninao uweka hapa Facebook.

Kuna watu wana pesa,wana kila kitu ila wana lia usiku na mchana hawa hitaji chochote isipokua #Kufarijiwa tu kutiwa moyo,na kuoneshwa upendo wa Mungu baadae wana amua hata kubadilika na kumfuata kristo.
Kama wewe una raha,hujawahi kulia,hujawali kupitia wakati mgumu usifikiri wanao pitia hawajuwi kuomba ao hawajuwi kutafuta ao hawana akili kama yako ao hawahitaji kuishi maisha ya raha kila leo kama wewe POA.ila elewa wana pitia na kwa kua ni mapito tu watavuka pia

Wanafiki wakubwa ninyi,chezeni na wale wasio jua ujanja wa shetani,chezeni na wale munao kaa nao kusengenya,tena chezeni na wale wasio jielewa na Ukisikia Unafiki wako umekuzidi na moyo wako umejaa hila,chuki,wivu ,ukabila...kila anacho kifanya mwengine kinakupa shida ,unajiona wewe ndio unajua sana,wengine wote ni 0,basi elewa una tatizo,ingia chumbani kwako,tulia ndani na umlilie Mungu aku badilishe #ANAKUWEZA bila hivo UTASUBIRI sana.

Leo nilitamani tu kukwambia kwamba :Tumeitwa na Mungu tofauti,kila mtu ki vyake,na historia zetu tofauti,aliko mtoa kila mtu ni tofauti na mwengine na anavyo tutumia Mungu ni tofauti ila wote ni kwa ajili tu ya kuujenga mwili wa kristo.#UMESIKIA

Comments