RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SUPER NYAMWELA AELEZA KUFUNDISHA DANSI KANISANI




Super Nyamwel.

MWANAMUZIKI wa Dansi, Hassan Mussa ‘Super Nyamwela’ ameibuka na kueleza kuwa haoni shida anavyofundisha kucheza ‘dansi’ kanisani kwani ndiyo kazi yake aliyoichagua.

Akibonga na Mikito Nusunusu, Nyamwela alisema licha ya kwamba ni muumini wa dini ya Kiislam amekuwa akiingia makanisa mbalimbali kufundisha wanakwaya kucheza hivyo haoni tatizo maana hawamlazimishi kusali wanavyosali wao.

“Ninafundisha kwaya katika makanisa mbalimbali jinsi ya kucheza na ninalipwa vizuri, sioni shida tena wakati mwingine naingia na kanzu yangu wala hakuna anayeniuliza kwa kuwa wanajua ninachofuata pale ni kazi tu,”alisema Nyamwela.

STORI: MIKITO NUSU NUSU

Comments