RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

19.11.2017: MAMA GLORY AMSHUKURU MUNGU KUPATA MTOTO


Mama Glory siku ya Jumapili 19.11.2017 katika ibada ya KUVIKWA KIBALI aliweza kumshukuru sana Mungu kwa kujifungua mtoto, na hivi ndivyo alivyosema, "Bwana Yesu asifiwe. Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kupata mtoto kwani kuna watu wengi sana wanapoingia hospitalinikujifungua hawatoki tena, lakini mimi Mungu alinipigania nilijifungua na nimzima na mwanangu anayeitwa Glory. Ninamshukuru sana Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa maombi aliyoniombea pamoja na wewe uliyeniombea. Mungu awabariki sana."

Pengine umehangaika sana kutafuta mtoto, umeenda kwa waganga, umezunguka makanisa mbalimbali na hujafanikiwa. Ndugu zako wanakusema kwa kutokuwa na mtoto, mume wako hakupendi tena, umekuwa ni mtu wa majonzi na masikitiko. Nikualike katika ibada ya Jumapili hii saa 3 asubuhi ili tumlilie Mungu ajibu haja ya moyo wako. Wengi wamefika katika ibada za Mlima wa Moto Mikocheni "B" na wamefanikiwa.












Comments