RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

26.11.2017: WATU WALIVYOMUABUDU MUNGU KATIKA IBADA YA KUTAMBUA NGUVU YA MUNGU ILIYOMO NDANI YA MUAMINI

TAFAKARI:
"Na majivuno ya mwanadamu yatainamishwa, na kiburi cha watu kitashushwa; naye BWANA, yeye peke yake atatukuzwa siku hiyo. -Isaya 2:17"

Siku ya Jumapili 26.11.2017 watu waliweza kumuabudu Mungu katika ibada ya KUTAMBUA NGUVU MUNGU ILIYOMO NDANI YA MUAMINI iliyofanyika ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Praise & Worship Team ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" iliweza kuongoza kipindi kizima cha kuabudu. Watu waliguswa na nguvu za Mungu kupitia nyimbo zilizojaa uwepo wa Mungu. Ilikuwa ni ibada ya aina yake, Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa jinsi alivyokuwa akihudumia watu kwa kiwango cha juu sana..

Wewe ambye ulikosa ibada hii tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii itakayoanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Mungu ana mpango na wewe kwahiyo jitahidi sana kufika kanisani. Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na jopo la wachungaji zaidi ya 12 wamejipanga kukuhudumia kiroho na kimwili.

Kanisa limeandaa uasafiri wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola.

Tony Enock











Mhe. Marry Mwanjelwa - Naibu Waziri wa Kilimo





























Comments