RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

26.11.2017: WATU WAZIDI KUTOA MAONI YAO KUHUSU KUSANYIKO LA WATOTO WA MUNGU LA SHILO 2017

Watu wazidi kutoa maoni yao kuhusu Kusanyiko la watoto wa Mungu la SHILO 2017 ambalo hufanyika mara moja tu kwa mwaka. Kwa mwaka 207 litaanza Desemba 3 hadi 10 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Siku hizi 8 zitakuwa ni siku za BWANA KUJIFUNUA TENA katika kazi yako, nyumba yako, ofisi yako, familia yako, masomo yako, mahusiano yako, huduma yako, na sehemu mbalimbali. Ni siku za Mungu kujibu haja ya moyo wako. Ni siku za kupokea baraka kutoka kwa Mungu kupitia watumishi wake kama vile Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Mch. Noah Lukumay, Bishop Dr. Dunstan Maboya, Mch. Paul Kuria kutoka Kenya, Mch Elias Madoshi, Mch. Sylvanus Komba na jopo la wachungaji wa Mlima wa Moto Mikocheni "B". Pia utabarikiwa na uimbaji kutoka Happy Kwaya, Joybringers Kwaya, Mch. Masanja Mkandamizaji na wenginwengi. Ibada siku ya Jumapili zitaanza saa 3 asubuhi na siku za wiki ni saa 9 alasiri. Usipange kukosa mtu wa Mungu. Ubarikiwe.


Comments