RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MAOMBI MAALUM YA KULIOMBEA SHILO TANZANIA YAFANYIKA KATIKA OFISI YA MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE

Maombi maalum kwaajili ya Kongamano la SHILO TANZANIA 2017 yafanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Kumbuka Shilo ni kusanyiko la watoto wa Mungu ambalo hufanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" mara moja tu kwa mwaka. Na mwaka huu Shilo itafanyika kuanzia Desemba 3 hadi 10 2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", muda ni saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana siku za Jumapili na siku za katikati ya wiki ni saa 9 mchana hadi saa 1 usiku. 

Mungu akutie nguvu uweze kufika kupokea muujiza wako kwani kwa siku hizi 8 BWANA ATAKWENDA KUJIFUNUA KWAKO kwa njia ya tofauti sana 1Samweli 3:21.

Wanenaji ni wengi sana na baadhi yao ni Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Mch. Noah Lukumay, Bishop Dr. Dunstan Maboya, Mch, Paul Kuria kutoka Kenya, Mch. Elias Madoshi, Mch. Sylvanus Komba na wengine wengi.


Mungu akubariki sana.








Comments