RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

24.12.2017: WATU WALIVYOMSIFU MUNGU KATIKA MAANDALIZI YA MKESHA WA KRISMASI KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

24.12.2017: MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B": KIPINDI CHA SIFA Martha Komanya alivyoongoza kipindi cha kusifu na kuabudu katika ibada ya maadalizi ya mkesha wa Krismasi iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Mlima wa Moto Mikocheni "B" jijinio Dar es Salaam siku ya Jumapili 24.12.2017. Watu walimtukuza Mungu kwa njia ya sifa wakiongozwa na mbeba maono Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Hakika uwepo wa Mungu ulitawala katika hekalu la Mungu na watu walishuhudia nguvu za Mungu juu yao.

Naibu Waziri Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (MB) naye aliweza kushiriki ibada hii ya maandalizi ya mkesha wa Krismasi.

Mpendwa wangu, ipo faida kubwa sana katika kumsifu Mungu kwa kumaanisha na sio kwa kuhimizwa au kulazimishwa na muongoza ibada. Unapopata nafasi ya kumsifu Mungu unapaswa kufanya kwa kumaanisha ndipo utaona ule uwepo wa Mungu juu yako. Usimsifu Mungu kwa kufuata mkumbo wa watu wengine kanisani au mahali popote pale. Unapokuwa kanisani unatakiwa kuweka mawazo yako na akili zako zote kwa Mungu, kwahiyo kila unachokifanya hakikisha kinaunganishwa na Mungu. Watu wengi wanapokuwa kanisani katika ibada ya kusifu wanakuwa wanamsifu Mungu kwa mazoea, na kile wanachokiimba hawakimaanishi wala kukifanyia kazi. Unapotamka maneno unayoyaimba unatakiwa kumaanisha sio kuropoka tu bila kuyafanyia kazi. Kila Neno unalotamka katika wimbo limaanishe na ikiwezekana lifanyie kazi katika maisha yako ya kila siku. Kama wimbo ni wa kumsifu Mungu basi msifu kwa kumaanisha, kama wimbo ni wakukuonya basi yale unayoyaimba yafanyie kazi katika maisha yako, kama wimbo ni wa kukufariji basi amini Mungu ndiye anayekufariji n.k.

Mungu wetu ni Mungu wa sifa, anahitaji kuona watu walio "serious" kwaajili yake. Unapoimba, unatakiwa kumuweka Mungu mbele na kujiona kama vile anakuona unapomuimbia. Hutakiwi kuhamasishwa au kulazimishwa katika kumsifu Mungu, hutakiwi kusubiri mtu akwambie imba kwa sauti au piga makofi au cheza kwa bidii. Unatakiwa kuyafanya hayo yote kutoka ndani ya moyo wako.

Mungu na akubariki sana. Tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana

Martha Komanya akiongoza kipindi cha sifa



Naibu Waziri Kilimo Mhe. mary Mwanjelwa (MB) (kushoto)  akiongea na Rose Rwakatare






 Naibu Waziri Kilimo Mhe. mary Mwanjelwa (MB) (kushoto)  akisalimiana  na Rose Rwakatare


Naibu Waziri Kilimo Mhe. mary Mwanjelwa (MB) (kushoto)  akiongea na Mch. Noah Lukumay














Comments