RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

24.12.2017: HIVI NDIVYO WATU WALIVYOFANYA MAOMBI KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" KATIKA MAANDALIZI YA MKESHA WA KRISMASI

Hivi ndivyo watu wa Mungu walivyofanya maandalizi ya mkesha mkubwa wa KRISMASI siku ya Jumapili 24.12.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alifanya maombi maalum kwaajili ya mkesha huu mkubwa ambao unafanyika Jumapili 24.12.2014 saa 4 usiku hadi alfajiri katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Wachungaji wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" waliungana na mbeba maono wa kanisa hilo Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kuwaombea watu wote waliofika katika ibada hiyo pamoja na wale wote ambao walikuwa majumbani wakijiandaa kuja katika mkesha wa usiku huu.

Naibu Waziri Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa naye aliweza kuungana na waumini wa kanisa hilo kwaajili ya kuukaribisha mkesha mkubwa ambao utafanyika leo Jumapili 24.12.2017 katika nyumba ya BWANA ya Mlima wa Moto Mikocheni "B". Aliwaomba watu wazidi kumtegemea Mungu kwa kila jambo na kuwaomba wazidi kumuomba Rais Dkt. John Magufuli katika uongozi wake.

Watu wa Mungu waliongozwa sala ya toba na kuweza kuungama dhambi zao na kuanza ukurasa mpya wa kumtegemea Mungu kila jambo.

Ibada ilitanda uwepo wa Mungu, watu waliona nguvu za Mungu katika kipindi hiki cha maombezi.

Yawezekana ulikosa ibada hii, tunakukaribisha usiku ya wa leo katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ili uweze kushiriki na wenzako kumshukuru Mungu kwa yale aliyokutendea kwa mwaka mzima, kumuomba Mungu kwa mwaka 2018, kuungama dhambi zetu, kumuomba Mungu ulizi kwa mwaka ujao. Pia tunakualika katika ibada ya Jumapili ya Krismasi 25.12.2017 ili uweze kusherekea siku ya kuzaliwa Yesu Kristo. Mungu na akubariki sana.

Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare




Mch. Noah Lukumay

















Mch. Antony Mwakibete













Comments