RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

24.12.2017: MAMA ALIYETEGWA NA WANAE WASOMI NA ENGINEER WA NDEGE KENYA ATENDEWA MUUJIZA

Mama mjane (mama Mwakajavale) ambaye amesomesha watoto wake na wengine ni ma-engineer wa ndege nchini Kenya, kwa muda mrefu amekuwa hakubukwi na watoto wake wala hawamjali kwa lolote wala hata kumjengea nyumba. Mama huyu ambaye kwa asili ni mtu wa Kyela Mbeya lakini aliolewa na Mkenya na kusababisha maisha yake yote kuishi Kenya. Lakini baada ya mume wake kufariki aliamua kurudi nchini kwake Tanzania alikozaliwa. Kutoka na kutokumbukwa na wanae ilimsababishi kukonda kwa mawazo na kupata kizunguzungu kwa mawazo

Akiongea kwa furaha alisema, baada kuhudhuria mikesha ya akina mama "singles" wa Mlima wa Moto Mikocheni "B" na kufanyiwa maombezi na Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ili Mungu aweze kuongea na wane wamkumbuke na kumjali. Mungu alijibu maombi yake na hivi sasa wanae wanamjali na kumsaidia. Mama huyu akiwa na imani ya ajabu sana alisema kuanzia sasa atanenepa na hajisikii kizunguzungu tena.

Yawezekana na wewe wanao hawakujali kwa lolote na umehangaika kuwalea na kuwasomesha. Nataka nikuhakikishie kuwa kupitia maombi ya mtumishi wake Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare utakwenda kukumbukwa sasa. Karibu Mlima wa Moto Mikocheni "B" Jumapili hii ufanyiwe maombi kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana, na pia siku za katikati ya wiki kuanzia saa 9 alasiri








Comments