RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

24.12.2017: WATU WALICHEZA MBELE YA MADHABAHU YA KANISA LA MLIMA WA MOTO KATIKA MKESHA WA KRISMASI

Baada ya kupata Neno la Mungu na kuombewa katika mkesha wa KRISMASI, waumini waliweza kumsifu Mungu kwa kucheza mbele ya madhabahau ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na jopo la wachungaji wa kanisa hilo hawakuwa walinungana na waumini hao kumrudishia utukufu Mungu kwa kucheza na kuimba. Hakika kilikuwa ni kipindi cha baraka sana, watu walishuhudia nguvu za Mungu ndani yao, na uwepo wa Mungu uliotanda kanisa zima.

Wewe ambaye ulikosa nafasi hii, bado unayo nafasi ya kumsifu Mungu katika ibada ya Jumapili hii ambayo itaanza mapema sana saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Ni siku ya kumtukuza Mungu, kumsifu Mungu, na kumrudishia sifa Mungu wetu kwa matendo makuu anayoyafanya katika maisha yetu.

Usipange kukosa ibada hii, kuna kitu utaondoka nacho ambacho kitabadilisha maisha yako. Njoo ukiwa na IMANI ya kutatuliwa shida zako kutoka kwa Mungu mwenyewe kupitia mtumishi wa Mungu Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Mungu wetu hajawahi kushindwa kwa lolote, na hilo unalodhani haliwezekana kwa Mungu linawezekana. Usipange kukosa kabisa. Mungu akubariki.








Comments