RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MUSIC VIDEO | ASHLEY NASSARY – NI NEEMA



Kwa mara ya kwanza leo kutoka jijini Dar es salaam nimekusogezea video iitwayo Ni Neema kutoka kwa mwimbaji mpya kwenye kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania anayefahamika kwa jina la Ashley Nassary, video hii imeongozwa na Director Jackson Joackim kutoka Blessing Studios.
Ni Neema ni wimbo wa shukrani unaozungumzia upendo wa Mungu kwa mwanadamu ambaye ameuona mkono wa Bwana ukitenda makubwa katika maisha yake na anasisitiza kuendelea kuwa naye siku zote na hata milele kwa maana nguvu zake, upendo wake hauchunguziki wala haupimiki, Ni Neema.
Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ambao nina imani utakubariki sana. Karibu!

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Ashley Nassary kupitia:
WhatsApp: +255 675 300 768
Facebook: Ashley Nassary
Instagram: @ashleynassary
Twitter: @ashleynassary

Comments