RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

21.01.2018: MCH. NOAH LUKUMAY AKIWAOMBEA WAUMINI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO NA WAGENI WALIOFIKA KUSALI KANISANI HAPO

MAOMBI YANALETA MAJIBU CHANYA, Jijengee Tabia ya kufanya maombi kila wakati.
Muombe Mungu naye atakujibu kwa wakati wake. Unapoomba uwe ni mtu wa IMANI. Unapaswa kuamini kile unachhomba ili kiweze kutokea katika maisha yako.

Mtu wa imani mara nyingi huamini kile anachokifanya kuwa kitaleta majibu CHANYA. Watu wa imani hukumbwa na majaribu makubwa ambayo hulenga kushusha imani yao, lakini mtu wa imani hupambana na roho hizo chafu kwa maombi. Kupitia maombi mtu wa imani huvuka majaribu na kuwa mshindi.

Siku ya Jumapili 21.01.2018 Mch. Noah Lukumay aliweza kuwaombea waumini na kuwatamkia baraka za mwaka mzima. `Tulishuhudia watu wakifunguliwa na kuwekwa huru katika mapito yao ya taabu.

Wewe ambaye hukubahatika kufika katika ibada hii, basi jitahidi Jumapili hii uwe hekaluni mwa BWANA ili uweze kuombewa na kukufungua katika mapito yako. Ibada itakayoanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Amini Jumapili hii BWANA atakwenda kufanya njia pasipo na njia.

Mch. Noah Lukumay

































Comments