RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

21.01.2018: MCH. PRISCA CHARLES JINSI ALIVYOONGOZA KIPINDI CHA SIIFA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI “B”

Tamani sana kumsifu Mungu ungali bado una pumzi. Mungu wetu ni Mungu anayependa kusikia sauti yako ikipaza sauti na kumsifu. Hata wewe unapenda sana kuona mtu akikusifu na sio kukutamakia mabaya, ndivyo hata Mungu wetu anavyopenda sana kuona watoto wake wakimsifu kwa yale anayowatendea katika maisha yao.

Kumbuka yakuwa kuna mambo mengi sana Mungu wa mbinguni amekupigania na anazidi kukupigania, kwahiyo anahitaji kusikia ukimsifu na kumwabudu kwa roho wa kweli. Unapokuwa kanisani kumsifu Mungu usimwangilie mwingine anamsifuje Mungu wake, unachotakiwa kufanya ni kujiunganisha na Mungu na kumsifu Mungu wako bila ya kuiga wengine wanavyomsifu Mungu. Usipende kulazimishwa kuimba au kupiga makofi bali fanya kutoka ndani ya moyo wako kwa bidiii. Mungu wetu anaangalia Roho yako kama kweli inamsifu Yeye au unaigizia wengine wakiwa wanamsifu Mungu. Msifu Mungu sio kwa kuiga bali fanya kutoka ndani ya moyo wako na kwa upendo.

Siku ya Jumapili 21.01.2018 kanisa zima la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa kutambua umuhimu wa kumsifu Mungu liliwezaa kutenga muda maalum kwaajili yakumsifu Mungu. Ibada ya sifa ilioongozwa na Mch. Prisca Charles na Praise & Worship Team ya Mlima wa Moto Mikocheni "B". Watu walipokea nguvu za Mungu kupitia kipindi hiki cha sifa na wengine kujazwa na Roho Mtakatifu. Hakika watu waliona ukuu wa Mungu kupitia sifa.

Wewe ambaye ulikosa ibada hii, tunakualika katika ibada ya Jumapili hii itakayoanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Itakuwa ni ibada ya kubadilisha historia ya maisha yako.

Kanisa limeandaa usafiri wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. Karibuni sana


Mch. Prisca Charles




Mch. Prisca Charles





















Comments