RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

21.01.2018: MHE. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AKIOMBEWA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI “B”

Maombi yana nguvu katika maisha ya Mkristo. Tamani sana kufanya maombi na washirikishe watumishi wa Mungu wakufanyie maombi. Kupitia maombi utaona milango yako wa mafanikio ikifunguliwa. Jitahidi sana kuwa mtu wa imani, kila unachoomba amini kimetokea. Imani yako ndiyo itakayokupa majibu ya maombi yako kutoka kwa Mungu. Usihofu kwa kile unachokiomba, kwani Mungu wako anauwezo mkubwa wa kukutimizia. Amini watumishi wa Mungu wanavykuombea kwani wao ni mabalozi wa Mungu hapa duniani. Mungu amewateua kwaajili ya kufanya kazi yake hapa duniani. 

Hata watumishi wa Mungu wanahitaji sana kufanyiwa maombi kwani nao ni binadamu kama sisi. Kwahiyo unapokuwa ukifanya maombi yako binafsi usisahau kuwaombea watumishi wa Mungu. Kumbuka hawa watumishi wa Mungu wamezungukwa na maadui wengi sana, na wanahitaji sana ulinzi kupitia maombi yako. Uombwa sana usiache kuwaombea watumishi wa Mungu ambao wamejitoa maisha yao yote kwaajili ya kukuimarisha kiimani ili siku moyo uweze kuona na Mungu wako wa mbinguni.

Siku ya Jumapili 21.01.2018 Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kutambua umhimu wa maombi aliweza kuapata nafasi na kufanyiwa maombi kutoka kwa wachungaji, watumishi wa Mungu mbalimbali na waumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Yawezekana unatamani sana kufanyiwa maombi na watu wengine lakini umekosa watu wa kukuombea. Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" limeandaa wachungaji wa kukuombea siku za katikati ya wikia katika ibada ya Jumapili itakayoanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana utapata nafasi ya kuombewa na Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Kwahiyo tunakualiaka sana katika ibada ya Jumapili hii.

Kanisa limeandaa usafiri wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola jijini dar es Salaam, Tanzania. Karibuni sana







Comments