RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

Cece Winans Ang’ara Tuzo Za Grammy 2018.

Hatimaye Tuzo Za Gramophone Award Ambazo Kwa Sasa Zimezoeleka Kama Grammy Awards Jana Tarehe 28 Jan Zilifanyika Madison Square Garden In New York City, Na Ni Mara Ya Kwanza Kufanyika Nje Ya Los Angeles Toka Mwaka 2013. Na Katika Gospel Ambapo Vilikuwepo Vipengele Vitano Tayari Washindi Wamepatikana.
Best Gospel Performance/Song


Tuzo Hi Hutolewa Kwa Mwimbaji Au Mwandishi Kwa Ajili Ya Wimbo Bora Wa Gospel Uliofanya Vizuri Na Walichaguliwa Waimbaji Wa Nne Na Kundi Moja Akiwemo Tina Campbell, Jj Hairstone, Leandria Johnson, Cece Winans Na The Walls Group Ambapo Cece Winans Ameibuka Mshindi Na Kuchukua Tuzo Hiyo.
Best Contemporary Christian Music Performance/Song

Tuzo Hii Hutolewa Kwa Mwimbaji Au Mwandishi Aliyefanya Vizuri Katika Nyimbo Zenye Mithili Ya Christian Pop, Christian Rap/Hip-Hop, Or Christian Rock Single Or Track. Na Nyimbo Zilizochaguliwa Kushiriki Tuzo Hizi Ni Pamoja Na Oh My Soul – Ulioimbwa Na Casting Crowns , Clean – Wimbo Huu Umeimbwa Na Kuandikwa Na Natalie Grant, What A Beautiful Name – Ambao Umeimbwa Na Kundi La Hillsong Worship, Even If – Ulioimbwa Na Mercyme, Hills And Valleys – Ulioimbwa Na Tauren Wells. Na Katika Tuzo Hizo What A Beautiful Name Kutoka Kwa Kundi La Hillsong Worship Umechukua Tuzo Hizo.


Best Gospel Album

Tuzo Hizi Hutolewa Kwa Album Ambayo Imeweza Kuchezwa Zaidi Ya Asilimia 51 Na Pia Kwa Kuwa Na Mauzo Mazuri Zaidi. Na Album Zilizochaguliwa Kushiriki Tuzo Hii Ni Crossover: Live From Music City

Travis Greene, Bigger Than Me – Le’Andria, Close – Marvin Sapp, Sunday Song – Anita Wilson, Let Them Fall In Love – Cece Winans, Na Album Iliyochukua Tuzo Hii Siku Ya Jana Ni Yake Cece Winans Let Them Fall In Love.

Best Contemporary Christian Music Album

Tuzo Hizi Hutolewa Kwa Album Ambayo Imewezwa Kuchezwa Zaidi Ya Asilimia 51 Na Iliyobeba Nyimbo Zenye Muundo Wa Pop, Rap/Hip Hop, Or Rock Recordings. Na Mwaka Huu Album Zilizokuwa Zinawania Album Hii Ni Pamoja Na Rise – Danny Gokey, Echoes (Deluxe Edition) – Matt Maher, Lifer – Mercyme, Hills And Valleys – Tauren Wells, Chain Breaker – Zach Williams Na Zach Williams Kwa Wimbo Wake Wa Chain Breaker Amwchukua Tuzo Hiyo.


Best Roots Gospel Album

Tuzo Hii Pia Hutolewa Kwa Album Iliyofanya Vizuri Na Kuchezwa Zaidi Ya Asilimia 51 Iliyobeba Nyimbo Zenye Mahadhi Ya Country, Southern Gospel, Bluegrass, And Americana Recordings. Na Album Zilizoshiriki Ni Pamoja Na Give Me Jesus – Larry Cordle, Resurrection – Joseph Habedank, The Best Of The Collingsworth Family – Volume 1 – The Collingsworth Family, Sing It Now: Songs Of Faith & Hope – Reba Mcentire, Na Hope For All Nations – Karen Peck & New River. Na Aliyechukua Tuzo Hii Ni , Reba Mcentire Na Album Yake Ya Sing It Now: Songs Of Faith & Hope.
Sherehe Ya Kwanza Ya Grammy Awards Ilifanyika Mei 4, 1959, Ili Kuheshimu Na Kuheshimu Mafanikio Ya Muziki Na Waimbaji Mwaka Wa 1958.

Comments