RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

DKT. MWANJELWA AISHUKURU CHINA KWA KUONYESHA NIA YA KUISAIDIA TANZANIA KWENYE MAENDELEO YA TAFITI ZA KILIMO CHA MINAZI NA MIHOGO

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa ameishukuru Serikali ya China kwa kuonyesha nia ya kusaidia eneo la utafiti na maendeleo hususan kwenye kuendeleza zao la minazi na mihogo kupitia Kituo cha Utafiti wa Mazao cha Mikocheni JIJINI Dar es Salaam.

Dkt Mwanjelwa amemshukuru Serikali ya China kupitia Naibu Waziri wa Kilimo wa China Dkt Qu Dongyu mara baada ya kufanya ziara katika Kituo hicho mapema leo.


Katika Wasilisho lake kwa ugeni wa Waziri huyo wa Kilimo kutoka China, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utafiti Mikocheni Dkt Fred Tairo amesema Kituo kimekuwa kikiendesha tafiti mbalimbali zenye lengo la kuzuia na kukabiliana na magonjwa hatari ya minazi na mihogo lakini kikwazo kikubwa kimekuwa teknolojia hafifu na uzoefu mdogo katika nyanja hiyo.

Mara baada ya wasilisho hilo Naibu Waziri wa Kilimo wa China ambaye anataaluma ya kilimo amesema Serikali ya China ipo tayari kuisaidia Tanzania kwenye maeneo ya utafiti wa kuzuia magonjwa ya mazao kwenye minazi na mihongo na kutoa wito kwa Watafiti wa Tanzania kuongeza juhudi katika kubunia teknolojia mbazo zitakuwa rahisi na rafiki kwa Wakulima wa Tanzania ili iwe rahisi kuziuza na baadae pato lake lisaidie Kituo hicho kujiendesha.

Dkt Qu Dongyu yupo nchini kwa ziara ya Kiserikali pamoja na Mwenyeji wake, Dkt Mary Mwanjelwa ambapo wote kwa pamoja wamepata nafasi ya kuitembelea maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni na kujionea matokeo ya tafiti mbalimbali.

Akizungumzia kuhusu uwezeshaji wa Serikali ya China kwa Kituo cha Utafiti Mikocheni, Mtafiti Mwandamizi wa Kituo cha Mikocheni Dkt Aloyce Kulaya amesema kwa sehemu kubwa Kituo kimekuwa kikipata uwezeshaji kutoka Serikalini pamoja na Wabia wa Maendeleo kama Mfuko wa Bill and Belinda Gates Foundation na kuongeza kuwa uwezeshaji kama kutoka Serikali ya China utaongeza tija na uzalishaji katika mazao mengine si kwa minazi na mihogo tu.

Dkt Qu Dongyu anataraji kumaliza ziara yake ya Kiserikali hapo kesho kwa kukutana na Wawekezaji wa China waishio Tanzania na baadae atareje nyumbani siku hiyo ya Jumamosi.

MWISHO.







Comments