RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

Matokeo Ya Kidato Cha Nne 2017 Yako Hapa. Shule Zilizofanya Vizuri Zatajwa.

Baraza la mitihani Tanzania NACTE limetangaza matokeo ya Kidato cha Nne na shule zilizofanya vizuri kwa mwaka 2017 ambapo Jumla ya watahiniwa 385,767 walisailiwa kufanya mtihani.


Akitangaza matokeo hayo leo mbele ya waandishi wa Habari, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde ametaja shule hizo kuwa kuwa ni St. Francis Girls, Feza Boys, Kemebos, Bethel Saabs Girls, Anuarite, Marian Gilrs, Canossa, Feza Girls, Marian Boys na Shamsiye Boys.

Hata hivyo, Dkt. Msonde ametaja shule 10 zilizofanya vibaya katika mtihani wa taifa ni : Kusini, Pwani Mchangani, Mwenge, Langoni, Furaha, Mbesa, Kabugaro, Chokocho, Nyeburu na Mtule.

Kwa urahisi unaweza kuyaona matokeo ya kidato cha nne kwenye link iliyoandikwa ‘CSEE 2017’ >>>CSEE 2017

Unaweza pia kuyatazama matokeo ya matokeo ya mtihani wa maarifa (QT) 2017 >>>(QT) 2016

Comments