RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

04.02.2018: MCH. PRISCA CHARLES AGUSA MIOYO YA WATU KWA UIMBAJI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

// ZABURI 148:1 Halleluya. Msifuni BWANA kutoka mbinguni; msifuni katika mahali palipo juu. Msifuni enyi malaika wake wote,; msifuni majeshi yake yote.//

Mungu wetu ni Mungu anayependa sana kuona viumbe alivyoviumba vinapata muda mzuri kwaajili ya kumsifu kwa yale anayoyafanya kwa viumbe vyake. Hata wewe unatamani kusikia mtu akikusifu kwa yale unayoyafanya. Hakuna mtu anayetamani kupokea sifa mbaya katika maisha yake. Kwahiyo ukitaka kubarikiwa na kumfurahisha Mungu wetu, basi anza zoezi la kumsifu Mungu wako kwa nyimbo, vinanda, makofi, vigerere na kwa kutamka maneno mazuri mbele ya Mungu wako. Unapomsifu Mungu wako unatakiwa kumsifu kutoka ndani ya moyo wako. Usiwe mtu wa kuiga mikumbo au kufuata watu wengi wanapomsifu Mungu wao, bali fanya kwa kumaanisha, onyesha mfano mpaka watu watamani kumsifu Mungu kama wewe. Usingoje mtu akulazimishe kupiga makofi, kucheza, kuimba kwa sauti, kupiga vigelele; unatakiwa kufanya mwenyewe kutoka ndani ya moyo wako. Acha tabia ya kuzoea ibada za sifa, bali kila wakati uione ibada ya sifa ni kitu kipya kwako.

Praise & Worship Team ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ikiongozwa na Mch. Prisca Charles iliweza kushirikiana na waumini wa kanisa hilo kwa kumsifu Mungu kwa njia ya nyimbo. Ibada hii ya kusifu ilifanyika siku ya Jumapili 04.02.2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.
Sasa tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii itakayoanza saa 3 asubuhi hadi saa 8n mchana. Kanisa limeandaa usafiri wa bure wa kufika kanisani kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola.
Jumapili hii Mungu anampango na wewe..USIKOSE

Mch. Prisca Charles


 




















































Comments