RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

11.02.2018: MHE. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE | Je, Unajua sababu ya kushushiwa heshima na wabaya wako?

Mhe. Bishop Dr. Getrude Rwakatare siku ya Jumapili 11.02.2018 katika ibada ya BIG SUNDAY TO REMEMBER 2018 iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na kuhudhuriwa na makanisa yote ya Mlima wa Moto Tanzania kuanzia saa 12 asubuhi hadi sa 12 jioni alikuwa na haya ya kusema, "Bwana Yesu apewe sifa, leo nataka nizungumze na wewe ambaye ulikuwa unaheshimika zamani ukiwa na kitu lakini sasa hivi huhesimiki tena kwasababu huna kitu kama zamani.

Kuna watu zamani walikuwa wanaheshimiwa na jamii, lakini hivi sasa hawaheshimiwi tena na jamii, sheatni kaondoa heshima yao na wanaonekana kama kituko mbele za watu. Lakini katika siku 21 za maombi tuliyofanya utakwenda kufunguliwa kwa jina la Yesu. Mungu ameshuka na majibu yako, na ni lazima uondolewe katika aibu yako. Ukisoma Mika 2:10 inasema, "Ondoka hapo ulipo mahali hapo sio pa hadhi yako". Mimi nimeona katika maono kuwa mahali ulipo sio pa "style" yako. Wewe unatakiwa uwe juu, unatakiwa kuwa mtu mwenye pesa.

Zamani ulikuwa na uwezo wa kifedha lakini sasa hivi huna uwezo. Lakini katika maombi ya siku 21 lazima unaenda kufanikiwa kwa jina la Yesu. Wewe ni mtoto wa Mungu lazima uishi kama mfalme, uwe na gari lako, nyumba yako, malazi mazuri, kula chakula kizuri.

Mimi kama mtumishi wako, nataka kukuondolea kila aina ya uhitaji katika jina la Yesu. Ninaong'oa uhitaji wa fedha, uhitaji wa chakula kizuri, uhitaji wa mafanikio, kila nguvu za giza zitoke kwa jina la Yesu.

Siku 21 za maombi ya Daniel, zina majibu matata na majibu hatari katika maisha yako. Kila pambo lililopandwa ndani yako ni lazima ling'olewe.

Kuna baadhi ya watu unawaona wanang'ara kwa nje lakini hali yao ya kiuchumi ni tete, shetani amenyang'anya kila kitu na hawaheshimiki tena na jamii. Lakini leo kwa jina la Yesu tunashughulika na watu waliomaututi kiuchumi. Klla mtu aliye kwenye "danger zone" leo ni lazima tumnasue kwa jina la Yesu., leo lazima Mungu akutembelee katika maisha yako, "Enough is Enough" ni lazima kieleweke katika maisha yako.

Kuna watu walio maututi kiafya, wana magonjwa yasioeleweka, wanafanyiwa "operation" lakini wakishafanyiwa hali yao inazidi kuwa mbaya.

Leo hii umekuwa mpweke, wakati zamani ulikuwa na marafiki, ulikuwa na "company" ya marafiki lakini sasa wamekuacha peke yako. Umekuwa ni mtu wa kuwaza, unatafakari mtu wa kukusaidia siku utakayopata matatizo. Leo tunaondoa hali ya upweke kwani upweke ni ugonjwa. Leo tunaondoa Roho ya kutopendwa na tunapanda roho ya kibali nadni yako kwa jina la Yesu. Watu wakikuona wakuite, jina lako liwe sukari midomoni mwa watu.

Ninaoma msichana aliyekataliwa kutokana na umri wake, kazi yake, umaskini wake, hali yake duni, elimu yake akipata mpenyo wa kibali kutoka kwa Mungu.

Watu dunia wanapoona mambo yao hauyaendi wanaenda kwa waganga wao, lakini watu wa Mungu hawaelewi wanapopatwa na magumu. Unapopatwa na magumu kama mtoto wa Mungu, wewe nenda kwa Mungu ukapate msaada na sio kwa waganga wa kienyeji watakutapeli tu. Kuna watu wa Mungu wanaponyang;anywa kazi wanaanza kusema, "Hapa kuna mkono wa mtu, ngoja niende kwa fundi yaani mganga wa kienyeji". Unatakiwa kusimama mbele za BWANA na kusema, "Leo ninang'oa magonjwa, umaskini, kutaliwa, kuonewa, kulogwa, kutupiwa majini." Ni lazima kama mtoto wa Mungu kujitetea.

Kuna watu katika maombi ya vita ya kung'oa shida zao, hawamaanishi, wanaomba kwa kulegalega. Unapofanya maombi ya vita unatakiwa kutomuonea huruma shetani, fanya kwa kumaanisha na kwa bidii.

Kwahiyo unatakiwa kushirikiana na Mungu katika kuuleta muujiza wako. Mungu ana nafasi yake na wewe una nafasi yako katika kuleta muujiza katika maisha yako. Unatakiwa kukataa kila roho ya umaskini, roho ya kufilisika, roho ya magonjwa kataa mabaya, jipandie mema.

KUJUA HAKI ZAKO
Ukisoma Mwanzo 26.18. Watoto ni lazima kujua haki zao mbele za baba zao. Isaka alijua haki yake mbele za baba yake Ibarahim. Alijua kuwa baba yake alikuwa akichimba visima na vilikuwa vinabubujika maji, lakini alipoenda katika visima vya baba yake akaona vile visima vimefukiwa na vifusi na maadui zake ambao ni Wafilisti. Isaka akaamua kuchimbua visima lakini kisima cha kwanza na cha pili Wafilisti waligombania bali alipochimbua cha tatu maji yalibubujika, watu na wanyama wakanywa wakafurahi.

Kisima ni wewe mtu wa Mungu uliyeumbwa na Mungu kwa mfano wake, unabubujika baraka, upendo, utu wema, msamaha, unabubujika mambo mazuri ya Mungu. Lakini leo hii shetani (Mfilisti) amekuja na akafukia vile visima vizuri, yale mambo yako mazuri ndani yako akaweka fitina, magovi, masengenyo. Lakini leo tunachimbua kwa koleo vile visima vilivyofukiwa na wabaya wako, tunapanda amani, furaha ndani yako kwa jina la Yesu...MUNGU NA AKUBARIKI SANA

Nikukaribishe katika ibada ya Jumapili hii itakayofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Kanisa limeandaa usafiri wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola.

Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare






























Comments