RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

JUMATANO YA UKOMBOZI WA MIKONO YAKO SI YA KUKOSA NDANI YA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Bwana Apewe Sifa: Nikualike katika ibada ya UKOMBOZI WA MIKONO YAKO itakayofanyika Jumatano hii katika nyumba ya BWANA Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 9 alasiri hadi saa 1 usiku.

Yawezekana unajitahidi sana kufanya kazi kwa bidii lakini huoni mafanikio kulingana na kazi unayofanya. Umri wako hauendani na mafanikio uliyonayo. Umri ni mkubwa, Mafanikio Kidogo.

Kuna watu wamefunga kazi ya mikono yako. Kuna watu wabaya wanaopenda kuona hufanikiwi. Kila kukicha wanakunenea mabaya katika kazi yako au huduma yako.

Jumatano hii tutakata minyororo iliyofunga mikono yako isizae matunda kulingana na kile unachokifanya. Ni siku ya kukombolewa kwako!!!

Mungu akusaidie Jumatano hii tukutane katika hekalu la Mungu, Mlima wa Moto Mikocheni "B". Soma Isaya 35:3 itakusaidia kutambua ibada ya UKOMBOZI WA MIKONO YAKO.

SUPERWOMAN
Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.
Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

Comments