RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

Mzee Wa Upako Awacharukia Mitume Na Manabii

Mchungaji Wa Kanisa La Maombezi (GRC) Lililopo Ubungo Jijini Dar, Lusekelo Antony Amewaongelea Watumishi Wanaojiita Mitume Na Manabii Huku Akidai Kuwa Wanatafuta Kuishika Saikolojia Ya Watu Kwa Sababu Majina Hayo Yanautisho.



Ameandika;

“Kwenye Biblia Utume Na Unabii Ni Miongoni Mwa Huduma Kuu Kubwa Na Tafsiri Ya Mtume Ni Mtu Aliye Tumwa Na Mungu Kuanzisha Imani Mahala Ambako Hakuna Hiyo Imani Na Sio Kuanzisha Zehebu Mfano Ni Kupeleka Ukristo Mahala Ambako Ukristo Haupo Hapo Ndipo Mtu Ana Sifa Ya Kuitwa Mtume. Sasa Hawa Watu Wanao Jiita Manabii Na Mitume Sikuhizi Wanacho Fanya Ni Kama Kujenga Msingi Juu Ya Msingi Wa Mtu Mwingine Maana Katika Swala La Mitume Huku Kwetu Ile Imani Ilishaletwa Tangia Zamani Na Wale Wa Mishonari Kipindi Hicho Imani Ya Kikristo Haikuwepo.




Watu Wengi Wanashindwa Kufahamu Hili Swala Kwamba Uchungaji Sio Cheo Ni Huduma Na Kadhalika Utume Na Unabii Sio Cheo Ni Huduma , Mfano Unaweza Mkuta Mtu Anajiita Mchungaji Hata Kanisa Analo Chunga Waumini Hana Sasa Hapo Uchungaji Uko Wapi ? Maana Uchungaji Ni Maisha Ya Kila Siku Ya Kuchunga Waumini Na Kazi Ya Mtume Ni Kupeleka Imani Mahala Ambako Imani Haipo , Baadhi Ya Watu Wanakimbilia Kujiita Mitume Na Manabii Ili Kucheza Na Saikolojia Za Watu Maana Hayo Ni Majina Yenye Utisho Kwa Mtu Akiyasikia. Mungu Atusaidie Sana.”

Comments