RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

23.03.2018: MANESA SANGA AGUSA MIOYO YA WATU KWA UIMBAJI KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"


//ZABURI 112: 1-2: Haleluya. Heri mtu yule amchaye BWANA, apendezwaye sana na maagizo yake. Wazao wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa.//

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kumtumia mtumishi wake Manesa Sanga ambaye alitubariki sana katika ibada ya MAOMBI YA KUKOMESHA ROHO ZA MAPOOZA iliyofanyika siku ya Jumapili 23.03.2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Kupitia nyimbo zake watu tulibarikiwa sana na kuguswa na nguvu za Mungu kwa ule ujumbe uliokuwa ukiimbwa. Hakika Mungu anamtumia sana mtumishi wake Manesa Sanga ambaye pia ni muumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Sasa, nikualike katika ibada ya MIUJIZA itakayofanyika Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Kanisa limekuandalia usafiri wa bure wa kufika kanisani kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola DSM.

Tunakuomba uje na mwenzako Jumapili hii.

Manesa Sanga









Comments