RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

23.03.2018: MHE. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AWAOMBEWA WATOTO WADOGO NA KUWATAMKIA BARAKA

Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 23.03.2018 katika ibada ya MAOMBI YA KUKOMESHA ROHO ZA MAPOOZA aliweza kupata kibali kutoka kwa Mungu cha kuweza kuwaombea watoto wadogo wote waliofika katika ibada hiyo pamoja na wazazi wao. Hii ilikuwa ni ibada ya namna yake kutokana ule muunganiko wa madhabahu na Mungu kupitia mtumishi wake. Watu waliguswa sana na uwepo wa Mungu na wingu la Mungu lililokuwa juu yao. Hakika Mungu alishughulika na maisha ya watoto hawa pamoja na wazazi wao. 

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa yale yote anyofanya katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B". Mungu amekuwa mwema kwa kila mtu anayeshiriki ibada za kanisa hili. Tunashuhudia watu wakifunguliwa kutoka katika vifungo vibaya vya shetani na kuwekwa huru baada ya kuombewa. Pia tunakushukuru sana wewe unayefika kuabudu nasi na kuwa "Member" wa kanisa hili la ISHARA na MIUJIZA. 

Yawezekana ulikosa ibada hii Jumapili, na ungetamani Mungu kupitia mtumishi wake Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ashughulike na maisha yke katika masomo yake, afya yake, kipaji chake, karama yake, maadili yake, tabia yake na mengine kama hayo; Basi usipange kukosa ibada ya Jumapili hii ambayo itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B"

kanisa limekuandalia usafiri wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. Tunakuomba sana uje na mwanao, mtoto wa jirani yako au ndugu yako, dada wa nyumbani mwako, rafiki yako, ndugu yako ili nao waweze kukutana na baraka za Mungu Jumapili hii. Kwa kufanya hivyo BWANA atakubariki na kukuinua KIROHO na KIMWILI. Ubarikiwe sana.
Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare




























Comments