RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

23.03.2018: WANAOHITAJI WATOTO WAKIOMBEWA NA MHE. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE

Katika maisha tunayoishi hapa duniani kila mtu anatamani siku moja awe na famili yake, azae watoto wa kike na wakiume, aishi maisha ya amani katika ndoa. Hakuna mtu anayependa kuishi maisha kutokuwa na mtoto au watoto, kila mtu anatamani kuwa na mtoto wake, hakuna mwanamke anayetamani kuishia maisha ya kutozaa au kutokuwa na uwezo wa kubeba mimba, hakuna mwanamke anayependa kuona mimba yake imeharibika na kuua kiumbe chake tumboni. Mwanandoa hasa mwanamke hapendi kuona mawifi zake, ndugu zae na majirani zake wanamdharau kwa kukosa mtoto, hakuna mtu anatamani kuona watu wanamsema maneno mabaya eti hazai au hana mtoto. Kila mtu anatamani kuwa na familia yake na watoto wake, kila mtu anatamani kusikia mtoto akimtania, kila mtu anatamani kuona mtoto akiwa karibu naye. Moja ya furaha ya wanandoa ni kuwa na familia na sio kuishi wawili tu yaani mume na mke. 

Ila kuna watu ambao kazi yao ni kuvuruga ndoa za watu, kuondoa amani katika ndoa, kusababisha ugomvi katika ya ndugu. Watu hawa wanakwenda kwa waganga na kuwatupia wana ndoa nguvu za giza ili wasizae, waishi maisha ya kugombana kati ya mume na mke au katika ya ndugu na mke.

Kwahiyo wale wanaotamani kuwa na watoto, nataka niwambie kuwa yupo Yesu Kristo mtenda miujiza anaweza kukupa mtoto. Huyu Yesu anachotaka kutoka kwako ni kumtii na kufuata maagizo anayokuagiza kupitia kitabu chake kitakatifu yaani Biblia. Pia unatakiwa kuwa karibu na watumishi wa Mungu watakaokusaidia kuinua imani yako, kukufariji, kukusaidia wakati wa shida na raha.

Siku ya Jumapili tumeshuhudia mtumishi wa Mungu Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akiwaombea wamama na wadada wenye uhitaji wa watoto. Ibada hii ya Maombi ya Kukomesha Mapooza ilifanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"siku ya Jumapili 23.03.2018.

Yawezekana na wewe umehangaika sana kutafuta mtoto bila mafanikio, yawezekana wasiokupenda wana kunenea maneno mabaya juu yako na juu ya uzao wako, yawezekana ulienda kwa waganga na wakakunenea maneno mabaya ya kutoshika mimba, yawezekana mimba unashika lakini hazikai, yawezekana unapata mimba na unazaa lakini mtoto hakai muda mrefu anakufa, yawezekana umebarikiwa kuwa na watoto lakini wamefanyika kuwa mizigo kwako na huna furaha ya kuwa na watoto, yawezekana, umekosa amani katika ndoa yako kwa kukosa watoto, yawezekana ndugu na marafiki zako wanakucheka na kukutukana kwasababu huzai. Ndugu yangu, yupo kimilio letu ambaye ni Yesu Kristo. Unatakiwa kumkubali huyu Yesu na kuyatii yale anayokuagiza kutoka katika Biblia au kupitia watumishi, kubali kutumika nyumbani mwa BWANA, shiriki ibada kila kuitwapo leo, uwe mtu wa maombi na kufunga, na fanya yale yanayompendeza Mungu.

Nikualike katika ibada ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Kanisa limekuandalia usafiri wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Cola Cola jijini Dar es salaam Tanzania.





























Comments