RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

28.03.2018: MCH. MBUNDA AGUSA MIOYO YA WATU KWA MAHUBIRI YAKE SIKU YA IJUMAA KUU


Siku ya Ijumaa Kuu ya Ibada ya kushiriki Meza ya BWANA yaani kunywa damu ya yesu na kula mkate iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" tulipokea Neno la Uzima kutoka kwa Mch. Mbunda wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Mungu alimtumia kwa njia ya tofauti sana. Watu walibarikiwa na upako aliokuwa anaachilia kutoka katika madhabahu ya Ishara na Miujiza ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Tunakuandalia video clip ya mahubiri yake ambayo utapata katika post hii hivi karibuni

Napenda sasa kukaribisha katika Ibada ya Jumapili ya Pasaka ya Kufufuka kwa BWANA wetu Yesu Kristo itakayofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakkatare. Ibada itaanza mapema saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Katika ibada hii kutakuwa na Neno la Mungu juu ya Kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo, maombi ya UFUFUO katika maisha yako yaliyofungwa na adui shetani usifanikiwe katiia kazi yako, biashara yako, ndoa yako, masomo yako, malengo yako, mahusiano yako, afya yako na mengine kama hayo, pia utatamkiwa baraka za Pasaka kutoka kwa Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, utapata mafuta yaliyoombewa na jopo la wachungaji 12 wa kanisa hilo, utaombewa shida zako, kwa asiyeokoka utaongozwa sala ya toba na kubatizwa kwa maji mengi na baada ya hapo utaanza masomo ya kukulia wokovu.

Kanisa limekuandalia usafiri wa bure kuanzia vituo vifuatavyo: Kituo Cha Mabasi Cha Makumbusho, Mwenge Kwenye Mataa Barabara ya Coca Cola, Ilala stendi, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/Mandela Road, Mbagala Rangi 3

..........................
// Mch. Mbunda
// Mlima wa Moto Mikocheni "B"
// Picha za ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Ijumaa.
//Tunawakaribisha wote siku ya Jumapili hii.

Mch. Mbunda



Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

















Comments