RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

28.03.2018: MHE. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE: WALOKOLE WENGI WA SASA WANAJISAHAU KUWA WAMEOKOKA

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa ibada ya Ijumaa Kuu ya Kushiriki Meza ya BWANA (Kunywa damu ya Yesu na kula mkate) iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Katika ibada hii Mhe. Bisho Dr. Gertrude Rwakatare alikuwa na haya ya kusema:-

WALOKOLE WENGI WA SASA WANAJISAHAU KUWA WAMEOKOKA
Watu wa dunia walisikia ya kwamba Yesu atafufuka siku ya tatu, wakaenda kuomba ulinzi juu ya kaburi ili washuhudie atakapofufuka, kwahiyo wakaomnba ruksa kwenda kulilinda kaburi ili waone huyu Yesu atatokaje kaburini. Kaburi la Yesu lilishindaliwe kweliweli. Lakini sisi watu wa Mungu mara nyingi tumekuwa tukisahau maneno ya muhimu aliyotuagiza huyu Yesu.. Tumeagiza kwenda ulimwenguni kote tukawafanye watu kuwa wanafunzi wa Mungu. Unajua sisi tuliokoka tunaangaliwa sana na watu wa dunia matendo yetu kwasababu sisi tumekataa kufanya maovu . Tuliyeokoka ni barua ya Mungu katikati ya mataifa. Lakini watu wa Mungu wa kizazi hiki wanajisahau sana, utakuta mlokole analipiza kisasi, mgomvi, mwenye hasira. Watu wa mataifa wanachunguza matendo yetu na mwenendo wetu wa wokovu kwahiyo wewe uliokoka unahitaji kuwa makini sana, na tabia yako ili kuulinda wokovu wako. 

KAMA MKRISTO, USIMWAIBISHE MWENZAKO MBELE ZA WATU .
Tunatafakari jinsi Yesu Kristo alivyotupenda, alikuwa tayari kuhimili mateso, matusi, aibu ili mimi na wewe tusipate mateso wala matusi wala aibu. Tafakari Yule Yusufu aliyeenda kuomba mwili wa Kristo ili akauzike kwenye kaburi lake jipya kwasababu aliona ni aibu Yesu kuzikwa mahali pale. Ukiona kuna watu wanataka kumuuza au kumuabisha ndugu yako au rafiki yako ili wapate pesa au wanufaike wao, basi unatakiwa kupamba nao ili kumstili aibu ndugu yako au rafiki yako. Pia ukiangalia Yule mume wake Bikira Maria (Yusufu) alijizuia kulala na mke wake kwasababu alikuwa na mimba ya siri, na hii alifanya ili asimwaibishe mke wake Bikira Maria. Kama wewe ni kristo wa kweli, hata kama unataka kufanya kitu kwaajili yako basi usimwaibishe mwenzako ili ufanikiwe, usimvue nguo mwenzako mbele za watu, usimwaibishe mwenzako mbele za watu, usimtupe mwenzako uliyeanza naye kama chuma cha moto. Ukitaka kufanya jambo lako na kuachana na uliyekuwa naye basi fanya jambo lako kwa hekima kwasababu unavyofanya kwa hekima unajenga mwili wa Kristo. Watu wanashangaa ulokole uko wapi kama watu waliokoka wanaaibishana wenyewe kwa wenyewe mbele za watu. Yesu aliabishwa sana lakini alivumilia kwaajili yetu na siku ya tatu alifufuka na kutoondolea aibu zetu.

UNATAKIWA KUMSTILI AIBU MWENZAKO HATA KAMA AMEKUKOSEA NA HUO NDIO ULOKOLE
Tunatakiwa kulistili aibu kanisa lako, unatakiwa kumstili mwenzako hata kama amekukosea. Fanya jambo lako kwa hekima bila kumuabisha mwenzako kwani sisi sote ni ndugu na ni damu moja yaani Damu ya Kristo ambayo ilitufanya kuwa watu wa Baba mmoja ambaye ni Mungu wa mbinguni. Ni lazima tupendane kwa upendo wa kweli, upendo wa dhati, upendo wa Agape na kwa njja hiyo watu watajua kuna ULOKOLE wa kweli. Kama sio hivyo tutahukumiwa na Mungu kwasababu tumekuwa tukiaibisha kazi yake tukiwa duniani. Watu wanashangaa sana wanapoona walokole wenyewe kwa wenyewe hatuelewani wala kufichiana aibu. Kama mlokole anakuwa tapeli watu watasema basin a huyu mwingine naye ni tapeli, na mwisho wa siku tunamuabisha Yesu Kristo. Sasa kwa kosa la walokole wachache tusiseme walokole wote wana tabia za ajabu ajabu. Wapo watu wa Mungu wanaomtumikia Mungu kwa hekima na maarifa

MAMBO YALIYOTOKEA WAKATI YESU ALIVYOFUFUKA
1. Kulikuwa na giza nene, kwasababu Mungu alikuwa anaficha aibu ya mwana wa Mungu aliye hai. Kwahiyo Mungu alistili aibu ya mtoto wake. Kwa kitendo hicho Mungu atastili aibu zetu, badala ya watu kukucheka Mungu ataificha aibu yako.

2. Tetemeko Kuu. Damu ya mwana wa Mungu ilivyogusa ardhi, basi ardhi ilikataa kupokea damu ya mwana wa Mungu asiye na hatia. Kulikuwa na tetemeko kuu mpaka wafu wakafufuka. Kwahiyo na wewe unata kumsulubisha Yesu kwa mara ya pili. Unajua kwa miaka ya sasa tunamsulubisha Yesu Kristo kwa kutenda dhambi, kwa kurudia matapishi, kwa kufanya vitu kama watu hatujaokoka, kwa kurudia mambo ya hiana. Tunatakiwa kuacha tabia hizo mbelle za Mungu
3. Pazia la Hekalu lilipasuka vipande viwiliviwili. Maana yake ni kwamba baada ya kufa Yesu Kristo kila mtu aliyekuwa anataka kutubu dhambi zake alikuwa anaenda moja kwa moja kwa Mungu na sio kupitia kwa mtu. Sadaka za zamani zilikuwa ni kuchinja mbuzi au kuku au ng’ombe kwa ondoleo la dhambi.

......................................................
// Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.
// Mlima wa Moto Mikocheni "B", Dar es Salaam, Tanzania.
// Ibada ya Kushiriki Meza ya BWANA (Mwilina Damu ya Yesu)
// Imefanyika Ijumaa 28.03.2018.
// Tunakualika katika ibada ya Jumapili katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana
//Kanisa limekuandalia usafiri wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola jijini Dar es Salaam.

Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare






















































Mch. Manumbu









Comments