RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

Natamani Sana Kuimba Nyimbo za Gospel-Maua Sama

Mwanadada anaetamba sasa hivi na kibao chake cha Nakuelewa Maua Sama amefunguka na kusema kuwa anatamani sana kuimba nyimbo za gospo kwa sababu mara nyingi amekuwa akijikuta akizisikia au kuimba anakuwa na raha sana.

Maua Sama ambae alitambulika zaidi na wimbo wake wa mahaba niue , amesema kuwa kila siku amekuwa anatamani sana kuimba nyimbo za kuhamasisha jamii na kwa jinsi anavyoona anatamani sana siku moja kuimba nyimbo za gospo na anahisi ipo siku ataimba tu kwa sababu ndicho kitu anachopenda pamoja na kwamba mwanadada huyo ni muislamu.

Comments