RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

01.04.2018: JINSI WATU WALIVYOMUABUDU MUNGU SIKU YA JUMAPILI YA PASAKA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Hivi ndivyo watu wa Mungu walivyomuabudu Mungu siku ya Jumapili ya Pasaka katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada ilikuwa na nguvu za Mungu na watu wengi sana walifunguliwa baada ya maombezi kutoka kwa Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.. 

Hakika Mungu anazidi kuonekana katika kanisa hili kupitia mtumishi wake Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na jopo la wachungaji 12 wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Tunashuhudia watu wakifunguliwa katika vifungo vya mateso, wakibarikiwa, wakiinuliwa imani zao, wakiwa na ile hofu ya Mungu, wakibarikiwa na kubwa zaidi wakiwa na upendo kama Yesu Kristo alivyotuagiza.

Katika ibada hii ya Jumapili ya Pasaka ya Ufufuo wa Vitu Vilivyokufa katika maisha ya watu, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt, Marry Mwanjelwa aliweza kushiriki ibada hii Takatifu na kuweza kulisalimia kanisa.

Wewe ambaye ulikosa kupokea baraka za Jumapili ya Pasaka, tunakualika katika ibada ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Hii itakuwa ni ibada ya kukuondoa katika hali yako ya uchungu na mateso na kwenda katika hali ya neema, baraka na mafanikio kwa jina la Yesu. Kitu cha kufanya ni wewe kuchukua maamuzi ya kufika hapa kanisani ukiwa na IMANI ya kupokea baraka za BWANA na kuondoka nazo.

Watumishi wa Mungu wamejiandaa kabisa kukuombea kwa Mungu ili ufunguliwe katika mateso uliyo nayo na pia ujifunze Meno la Mungu litakalokusaidia kusimamia wokovu wako. 

Huu ni wakati wako wa kumtumikia Mungu, huu ni wakati wa kufanya kazi ya Mungu, huu ni wakati wa kusimama na Mungu, huu ni wakati wa kumlilia Mungu, huu ni wakati wa kujikana kwaajili ya Mungu, huu ni wakati wa kutangaza Injili, huu ni wakati wa kusema na Mungu. Mtu wa kufanya hayo yote ni wewe na mimi, kwahiyo naomba Jumapili hii tuungane na wana Mlima wa Moto Mikocheni "B" kufanya kazi ya Mungu ili watu waokoke, wamjue Mungu, wafunguliwe na siku ya mwisho wa kuishi hapa duniani wakamuone MUNGU aliye hai kupitia huduma yako. Ukifanya hivyo Mungu atafungua milango ya baraka katika maisha yako.

Kanisa limekuandalia usafiri wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola jijini dar es Salaam Tanzania.

Tunakuomba sana uje na rafiki yako, ndugu yako, jirani yako ili naye apokee muujiza utakaupokea katika ibada ya Jumapili hii hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare







































Comments