RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

02.04.2018: MGENI RASMI WA TAMASHA LA MEGA MKATE NA PRAISE POWER 99.3FM AKIONGEA NA WASIKILIZAJI NA WADAU WA PPR- SINZA DAR ES SALAAM

Siku ya Jumatatu ya Pasaka ya Mega Mkate na Praise Power Radio 99.3FM, Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo lililofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kenton iliyopo Sinza Afrikasana jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hili lilikusanya watu wengi sana kutoka katika kila kona ya jiji la Dar es Salaam kwaajili ya kumtukuza Mungu na kumsifu. Katika tamasha hilo kuliwa na waimbaji wa nyimbo za Injili zaidi ya 30, kulikuwa ni michezo ya watoto, Neno la Mungu na Maombezi kupitia mtumishi wake Mhe.Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kama utakavyoona katika video. Tamasha hili liliandaliwa na kituo cha redio cha Praise Power Redio 99.3FM ambacho kipo chini ya kanisa la Mlima wa Moto Mikochenin "B" kwa Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Hili tamasha likuwa ni kwaajili ya watu wote na wasikilizaji wa Praise Power Radio, bila kujali dini zao, makabila yao, mataifa yao, umri wao, rangi zao, jinsia zao.

Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliwaomba Watanzania kufanya kazi kwa bidii na kumtumikia Mungu kwa mali zao na akili zao zote. Alitamani watu angalau kumfikia yeye kimafanikio au kufika robo ya mafanikio yake kwasababu hapendi kuona watu wakiwa na maisha magumu uku wakimtumikia Mungu. Aliwaomba watu kujituma katika kazi, kumtegemea Mungu na kumuomba Mungu, kushiriki ibada na kufanya mambo mema ya kumpendeza Mungu.

Baada ya kuhubiri Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kuwaombewa watu wote waliofika katika viwanja hivyo na kuwatamkia baraka. Na pia aliweza kuliombea Taifa la Tanzania pamoja na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Mwisho aliwaomba watu kushiriki ibada za kila Jumapili katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" zinazoanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.




























































































Comments