RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

02.04.2018: UONGOZI WA PRAISE POWER RADIO 99.3FM UKIONGEA NA WASIKILIZAJI KATIKA TAMASHA LA MEGA MKATE NA PRAISE POWER

Kamati na uongozi wa Praise Power Radio wakiongea na wadau na wasikilizaji wa Praise Power Radio katika Tamasha la Mega Mkate na Praise Power 99.3FM lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kenton maeneo ya Afrikasana, Sinza jijini Dar es Salaam Tanzania. 

Tamasha hili ambalo hufanyika mara moja tu kwa mwaka lilihudhuriwa na waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili Tanzania na Congo. Katika tamasha hili kulikuwa na michezo ya watoto, burudani mbalimbali, uimbaji, Neno la Mungu, Maombezi na pia kufahamiana zaidi.

Mgeni Rasmi alikuwa mmiliki wa kituo hiki cha radio Mhe. Bishop[ Dr. Gertrude Rwakatare ambaye aliwashukuru wasikilizaji na wadau wa Praise Power Radio na baadae alifundisha Neno la Mungu, alifanya maombi na mwisho aliwatamkia baraka.

Lengo kuu la tamasha hili likuwa ni kukaa karibi na wasikilizaji wa Praise Power Radio na kufurahi pamoja kama watumishi wa Mungu kwasababu Praise Power Radio ni kwaajili ya watu wote bila kujali dini, kabila, rangi, taifa, jinsia wala umri. Na ni redio inayosikilizwa na watu wengi sana kutokana na vipindi vya bora.

Mch. Alex Mapanga



























Comments