RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

Mwalimu Mwakasege Atoa Onyo Kali, Asema Jambo Hili Analifuatilia Kisheria.

Mwalimu Na Mtumishi Wa Mungu Christopher Mwakasege Atoa Onyo Na Taarifa Kali Kwa Umma Kwa Watumiaji Wote Wa Mitandao Ya Kijamii Akiwataka Watu Kuwa Makini Kutokana Na Udanganyifu Unaoendelea Huku Likitumiwa Jina Lake.
Katika Page Yake Facebook Ameandika;

“Bwana Yesu Asifiwe!
TAHADHARI!!!! Kuna mtu amefungua akaunti ya Facebook kwa jina la Christopher Mwakasege na ikiwa na picha zetu. Na ametaka watu wachangie uanzishwaji wa kituo cha redio. Tunakutarifu kuwa:
1. Akaunti hiyo siyo yetu, na hatujatuma mtukuifungua
2. Huyo mtu anajifanya mtunza hazina wetu ni mwongo na mwizi. Hatuna mtu wa namba hiyo ya 0765 681693 katika ofisi yetu. Na jina lake alilotumia kusajiri namba hiyo ni Lengine Moll. Sisi hatuna mtu wa jina hilo kwenye ofisi yetu.
3. Fedha zikitumwa huko hatuhusiki nazo.
4. Tunalifuatilia jambo hili kimaombi na kisheria.
Mtaarifu na mwingine ile asije akadanganyika.“

Comments