MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MZEE WA UPAKO AMJIBU ALIKIBA: “ACHENI UZINZI” – VIDEO


SIKU chache baada ya Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar, Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ kumnanga mwanamuziki Alikiba kuwa ana maringo, tofauti na Diamond Platnumz ambaye alidai kuwa ni mtu mwenye upendo na watu wote, kiongozi huyo wa kidini amerusha dongo jingine akiwataka wasanii kuacha uzinzi.

GLOBAL TV imefanya mazungumzo na Mzee wa Upako ambaye amesema msanii anatakiwa kuwa na adabu huku akitoa mfano kwamba Kiba anapoulizwa maswali hujibu kwa madaha, tofauti na Diamond ambaye alisema hujibu kistaarabu.

“Wasanii wanatakiwa kuacha uzinzi, sio leo una mke huyu kesho unamke mwingine, utakufa. Walikuwepo wasanii wengi tu lakini jiulize nini kiliwashusha hadi wakapotea, tumeona wasanii wengi, usijione wewe ndiyo wewe,” alisema Mzee wa Upako.

Hata hivyo, Mzee wa Upako alisema kwamba wasanii hao wawili ni kama watoto wake, hivyo hawezi kubishana nao mitandaoni.

Aidha, katika kutambua uwepo wa muziki wa kizazi kipya alisema wapo wasanii wengi anaowafahamu na wanaofanya vizuri nchini na si Kiba na Diamond pekee, wamewataja wengine kuwa ni Ben Pol, Mrisho Mpoto ‘Mjomba’, Darasa na wengine.

Wakati huohuo, katika ujumbe ambao Alikiba aliuweka katika akaunti yake ya Twitter, amemtaka kiongozi huyo wa dini ajikite katika shughuli zake na aache kufuatilia mambo yake.
0