RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

Kashfa ya ngono yawalazimu Maaskofu 34 wa Kikatoliki kujiuzulu




Leo May 19, 2018, Maaskofu 34 wa Kanisa katoliki nchini Chile wamemuomba Baba Mtakatifu, Papa Francis kuridhia kujiuzulu nafasi zao kutokana na kashfa iliyowaandamana ya udhalilishaji wa kingono uliodaiwa kufanyiwa vijana wadogo wa kiume nchini humo.

Kabla ya kufikia uamuzi huo, maaskofu hao waliwaomba radhi waathirika wa vitendo hivyo pamoja na kanisa kwa “makosa makubwa waliyoyatenda”.


Bado haijafahamika mara moja iwapo Papa amekubaliana na ombi hilo la kujiuzulu ama la.


Amekuwa katika kukosolewa nchini Chile kwa uamuzi wake wa kumteua askofu ambaye alishutumiwa na kamati ya makasisi kuhusika na kulinda vitendo vya udhalilishaji wa kingono nchini humo.

Alipofanya ziara nchini Chile, Papa aliuambia umma wa wakatoliki walifika kumlaki kuwa anajisikia “maumivu na aibu” juu ya kashfa hiyo iliyolikumba Kanisa la Katoliki nchini Chile.

Comments