RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

Askofu mwenye Wake 24 na Watoto 149 amehukumiwa kifungo





Leo June 28, 2018 Nakusogezea stori kuwahusu Viongozi wawili wa dini, mmoja akiwa askofu nchini Canada wamehukumiwa kifungo cha ndani (house arrest) pamoja na kipindi cha uangalizi, kwa kosa la kuoa wanawake wengi na kuzaa watoto wengi.

Shirika la habari la AP, limeripoti kuwa Askofu Winston Blackmore na mwenzake James Oler walikutwa na hatia mahakamani tangu July mwaka jana lakini wiki hii wamehukumiwa.

Blackmore ana wanawake 24 pamoja na watoto 149 huku Oler akiwa na wanawake watano.

Mahakama imemhukumu Blackmore mwenye miaka 61, kifungo cha ndani ya nyumba kwa miezi sita pamoja na mwaka mmoja wa kipindi cha uangalizi (probation).

Wakati huohuo, Oler mwenye umri wa miaka 53 amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu cha ndani ya nyumba pamoja na mwaka mmoja wa uangalizi.

Mbali na hukumu hiyo, Mahakama hiyo imempa adhabu Blackmore ya kufanya kazi za kijamii kwa saa 150 pamoja na Oler saa 75.

Awali, wawili hao walikuwa wanakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela.

Gazeti la nchini humo la Globla News, limeripoti kuwa Blackmore alianza kuwaoa wake zake tangu miaka zaidi ya ishirini iliyopita.

Imeelezwa kuwa alipokuwa anawaoa wanawake hao, wanawake 10 aliwaoa wakiwa na umri wa miaka 17, watatu walikuwa na umri wa miaka 16 na mmoja alikuwa na umri wa miaka 15.

Katika utetezi wao, wamedai kuwa wameonewa kwani walikuwa wanafanya jambo ambalo linakubalika kwenye imani yao.

Walikuwa wakifanya kazi kama maaskofu wa kanisa linalofahamika kama ‘Fundamentalist Church of Jesus Christ of Latter-Day Saints’

Comments