RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

Wanawake wagombana Kanisani wakigombea kukaa karibu na Mchungaji



Leo June 15, 2018 kuna hii ya kuifahamu Wanawake wawili nchini Kenya wamewashangaza wengi baada ya kuzozana na kukabana koo kanisani mbele ya Waumini wenzao wakigombania kukaa karibu na Mchungaji wa Kanisa hilo.

Inaelezwa kuwa mwanamke mmoja ambaye alifika kanisani akiwa amechelewa aligundua kuwa Mwanamke mwingine alikuwa ameketi katika kiti alichozoea kukaa ambacho kipo karibu na Mchungaji wa Kanisa lao.

Taarifa zinasema kuwa Mwanamke huyo alimwendea Mwanamke aliyekuwa amekaa karibu na Mchungaji na kumtaka anyanyuke ili akae kitu kilichoamsha mzozo na kuzaa ugomvi mbele ya Waumini wenzao.

Imeelezwa kuwa waumini ambao walibaki wanawashangaa ilibidi waingilie kati kuzima ugomvi huo huku wakidai kuwa waumini hao wanaliaibisha Kanisa lao.

Aidha kwa mujibu wa duru za kuaminika hazijaeleza kama Mchungaji huyo ana mahusiano na Wanawake hao.

Comments